DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, July 23, 2012

ZIARA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI, MHE. DKT. MARY NAGU (MB) KUKAGUA MAANDALIZI YA KILIMO CHA ZABIBU KWA NJIA YA MATONE KINACHOTARAJIWA KUENDESHWA NA LUBALA SACCOS ILIYOPO KATA YA LAMAITI HALMASHAURI YA WILAYA YA BAHI-DODOMA.

UNANISIKIA MWENYEKITI!
Waziri Nagu (aliyevaa miwani) akimsisitiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mhe. Hussein Kamau kufuatilia ahadi aliyoitoa ya kuishawishi Benki ya Uwekezaji (TIB) kutoa mkopo wa shilingi 1,349,463,000.00 kwa SACCOS hiyo. Fedha hizo zimeombwa kwa ajili ya kufanya tafiti za kihandisi (Engineering Design) na kuweka miundombinu ya umwagiliaji ambayo itahusisha mashine za maji, mashine za kuchanganya dawa, nyumba ya mashine, bwawa la maji na kutandaza mipira ya maji (Water drip system na fedha zinazobaki ni kwa ajili ya upatikanaji wa shamba.
Waziri wa Nagu (aliyepunga mkono) akiwashukuru wananchama wa LUBALA SACCOS kwa kumpa zawadi ya mbuzi wa maksai. Aidha, wana-LUBALA SACCOS wamempatia uanachama namba 91 ikiwa ni pamoja na kumlipia ada na kiingilio cha hisa pamoja na shamba lenye ukubwa wa ekari mbili (2).  

 Waziri Nagu akikabidhiwa mbuzi aliyezawadiwa na wanachama wa LUBALA SACCOS.

UMOJA WENU NDIYO NGUZO YA MRADI!

Waziri Nagu akiwahutubia wakulima ambao ni wanachama wa LUBALA SACCOS iliyopo Kata ya Lamaiti, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.

TUNAELEWANA JAMANI!

 

TAARIFA!

Afisa Mtendaji wa Kata ya Lamaiti, Ndg. Pascal Mangwela, akisoma taarifa kwa Waziri Nagu (Hayupo pichani) kuhusu  maandalizi ya mradi wa kilimo cha zabibu Kata ya Lamaiti.

SALAMU!

Waziri Nagu akisalimiana na akina mama ambao ni wanachama wa LUBALA SACCOS mara baada ya kukagua maandalizi ya shamba la wakulima hao.


WAMEJITAHIDI!

 1
 2
 3
 4
Picha namba 1,2,3 na 4: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akikagua maandalizi ya shamba la zabibu kwa njia ya matone pamoja na baadhi ya wanachama wa LUBALA SACCOS.






 1
 2
Picha namba 1 na 2: Maandalizi ya awali ya shamba la zabibu kwa njia ya matone yaliyofanywa kwa nguvu ya wananchi ambao ni wakulima wanaounda LUBALA SACCOS ambapo kwa pamoja wameweza kufyeka vichaka, kung'oa visiki, kusimamia upimaji, kukata mambo na kuandaa shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 200. Kazi hiyo imegharimu shilingi 26,390,000 milioni zikiwa ni nguvu kazi.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akipata maelezo na ya utangulizi kuhusu shamba kutoka kwa  Diwani wa Kata ya Lamaiti Mhe. Donaldi Mejiti (Mwenye shati la blue). Nyuma katika ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mhe. Hussein Kamau.

KARIBU SANA MHESHIMIWA!

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji (W) Bahi mara baada ya kuwasili katika shamba linalomilikiwa na LUBALA SACCOS lililopo Kata ya Lamaiti tayari kukagua maandalizi ya kilimo cha zabibu kwa njia ya matone. LUBALA ni kifupisho cha Lukali, Bankolo na Lamaiti ambavyo ni vijiji vinavyounda kata ya Lamaiti hivyo ni SACCOS ya kata.

Tuesday, May 15, 2012

MAFUNZO YA MADIWANI YANAENDELEA LEO!


Mwazeshaji wa mafunzo ya madiwani kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma, Bogit Samhenda akiwasilisha mada kwa washiriki hao kuhusu sifa na mwenendo wa Diwani ambapo ndani yake walifundishwa kanuni na maadili ya madiwani, Stadi za mawasiliano kwa Diwani kama KIONGOZI na siyo BWANA MKUBWA/MHE. Mafunzo hayo ya siku tatu yanayosimamiwa na OWM-TAMISEMI yanaendelea katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma kwa siku ya pili.

Monday, May 14, 2012

MAJADILIANO BAADA YA KUPIGWA MSASA

MAJADILIANO BAADA YA KUPIGWA MSASA

                                        1
                                         2
                                         3
                                         4
                                         5
PICHA NAMBA 1, 2, 3, 4 & 5. Waheshimiwa Madiwani ambao ni washiriki wa mafunzo ya Madiwani wakijadiliana na kufanya kazi katika makundi baada ya wawezeshaji kuwasilisha mada tatu aambazo ni:- Mfumo wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Wajibu na Majukumu ya Diwani na Utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa. Mafunzo hayo ya siku tatu yanaratibiwa na Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ambayo ni miongoni mwa mafunzo yanayosimamiwa na OWM-TAMISEMI katika Halmashauri zote nchini.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mhe. Hussein Kamau (aliyesimama) akisema maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya mteule wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Mkwasa kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Madiwani yanayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) katika Halmashauri zote nchini kupitia Sekretarieti za Mikoa. Kwa mujibu wa ratiba Halmashauri ya Wilaya ya Bahi inafanya mafunzo hayo ya siku tatu kuanzia leo tarehe 14/05/2012 hadi 16/05/2012 katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma.

Mkuu wa Wilaya mteule wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Mkwasa akifungua Mafunzo ya siku tatu ya Madiwani yanayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) katika Halmashauri zote nchini kupitia Sekretarieti za Mikoa. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mkwasa aliwaasa madiwani kupitia mafunzo watakayo pata wawe na mbinu za utendaji katika kukabiliana na umaskini, UKIMWI, ukosefu wa ajira na kudumisha amani ili kuweza kuleta maana ya maendeleo ya kiuchumi ya mahali husika (Local Economic Development).                                            

 1
 2
3

PICHA NAMBA 1, 2 & 3 ni Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Menejimenti ya Serikali za Mitaa, Emmanuel Kuboja akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Serikali za Mitaa wakati wa Mafunzo ya Madiwani leo kwenye ukumbi wa Manispaa Dodoma.

Wednesday, April 25, 2012

Mzee wa DomLand sasa nipo hewani kama kawa nimerudi kwa kasi ya kimbunga cha Tsunami katika tasnia ya KUHABARISHA tuwe pamoja