Tuesday, May 15, 2012
Monday, May 14, 2012
MAJADILIANO BAADA YA KUPIGWA MSASA
MAJADILIANO BAADA YA KUPIGWA MSASA
1
2
3
4
5
PICHA NAMBA 1, 2, 3, 4 & 5. Waheshimiwa Madiwani ambao ni washiriki wa mafunzo ya Madiwani wakijadiliana na kufanya kazi katika makundi baada ya wawezeshaji kuwasilisha mada tatu aambazo ni:- Mfumo wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Wajibu na Majukumu ya Diwani na Utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa. Mafunzo hayo ya siku tatu yanaratibiwa na Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ambayo ni miongoni mwa mafunzo yanayosimamiwa na OWM-TAMISEMI katika Halmashauri zote nchini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mhe. Hussein Kamau (aliyesimama) akisema maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya mteule wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Mkwasa kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Madiwani yanayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) katika Halmashauri zote nchini kupitia Sekretarieti za Mikoa. Kwa mujibu wa ratiba Halmashauri ya Wilaya ya Bahi inafanya mafunzo hayo ya siku tatu kuanzia leo tarehe 14/05/2012 hadi 16/05/2012 katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Wilaya mteule wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Mkwasa akifungua Mafunzo ya siku tatu ya Madiwani yanayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) katika Halmashauri zote nchini kupitia Sekretarieti za Mikoa. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mkwasa aliwaasa madiwani kupitia mafunzo watakayo pata wawe na mbinu za utendaji katika kukabiliana na umaskini, UKIMWI, ukosefu wa ajira na kudumisha amani ili kuweza kuleta maana ya maendeleo ya kiuchumi ya mahali husika (Local Economic Development).
12
3
PICHA NAMBA 1, 2 & 3 ni Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Menejimenti ya Serikali za Mitaa, Emmanuel Kuboja akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Serikali za Mitaa wakati wa Mafunzo ya Madiwani leo kwenye ukumbi wa Manispaa Dodoma.
Subscribe to:
Posts (Atom)