DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, October 17, 2013

SIKU YA CHAKULA DUNIANI OKTOBA 16, KITAIFA WILAYANI HANANG MANYARA YAFANA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Sera, Stephen Wasira (katikati) akipatiwa maelezo kuhusu kilimo bora cha maboga kutoka kwa Bi. Anjelina Ilonga (kulia) wa kikundi cha wakulima wa Mogitu Wilayani Hanang wakati wa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika kitaifa jana wilayani humo.

Kikundi cha burudani cha tarumbeta cha wasichana wa Shule ya Sekondari Madunga  iliyopo wilayani Mbulu Mkoani Manyara wakitumbuiza wakati wa sherehe za Siku ya Chakula Duniani zilizofanyika kitaifa wilayani Hanang mkoani humo jana. Kundi hilo lilikuwa kivutio kikubwa kwa umahiri wa kupiga tarumbeta.

Katibu wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) akiserebuka pamoja na watendaji wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na viongozi wa mkoa wa Manyara wakati wa sherehe za Siku ya Chakula Duniani zilizofanyika kitaifa jana wilayani Hanang mkoani Manyara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera na Uratibu, Stephen Wassira (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Rehema Nchimbi (kushoto) kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo kitaifa yalifanyika jana Wilayani Hanang mkoani Manyara. Waziri Wassira ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.

Wananchi wa wilaya ya Hanang waliojitokeza kwenye sherehe ya Siku ya Chakula Duniani iliyofanyika kitaifa jana Wilayani humo.

Wananchi wa wilaya ya Hanang wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwenye sherehe ya Siku ya Chakula Duniani iliyofanyika kitaifa jana Wilayani humo.

No comments:

Post a Comment