Kikosi kipya cha majeshi ya umoja wa Afrika kinafanya mazoeozi yake ya kwanza hii leo nchini Afrika Kusini.
Mazoezi hayo yanalenga kutathmini utayari wa kikosi hicho kutumika
wakati kunapotokea dharura na kunahitajika kikosi cha mbele
kitakachodhibiti hali na kuokoa maisha ya watu.
Lakini swali ibuka ni je jeshi hilo litatumwa katika taifa lililochangia wanajeshi wake ?
Mwandishi
wa BBC anayeshughulikia maswala ya kiusalama Tomi Oladipo, anasema kuwa
madhumuni ya kikosi hicho cha wanajeshi 25,000 kutoka mataifa ya bara
Afrika ni kupunguza kutegemea kwa majeshi ya mataifa ya ulaya kuja humu
barani kusuluhisha migogoro inayotokea.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza oparesheni yake ya kwanza mwezi januari mwakani.
Hata hivyo umoja wa Afrika unasema unahitajika takriban dola bilioni moja kufadhili shughuli na oparesheni za kikosi hicho.
Mwandishi
wa BBC anayeshughulikia maswala ya kiusalama anasema kuwa kuna
changamoto za ukosefu wa ushirikiano mwema baina ya mataifa shirika. |
No comments:
Post a Comment