DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, March 24, 2015

KINANA AWATAKA VIONGOZI WEZI, MAFISADI KUNG'OKA CCM HARAKA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake ukiwa umezingirwa na wananchi wa jamii ya kimasai ulipokuwa ukiondoka baada ya kuhutubia mkutano katika Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Kia, Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro jana, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadiu na Uenezi, Nape Nnauye, ameutaka uongozi wa Kampuni ya Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kuacha kuwabughudhi wananchi wa kata hiyo, baada ya kutoa mallamiko kuwa unataka kuwapora ardhi iliyo karibu na uwanja huo yenye ukubwa wa zaidi ya hekali 10,000 inayomilikiwa na vijiji 11. Komredi Kinana amekemea tabia hiyo ya baadhi ya viongozi wanaopora kinguvu ardhi za wananchi. Pia amewahakikishia wananchi hao kuwa atasaidia kurejesha ardhi hiyo kwa kukutana na Rais Jakaya Kikwete na kumwambia juu ya dhulma hiyo. Komredi Kinana , amesema kuwa kiongozi yeyote aliyeingia CCM kwa minajiri ya kutaka kujineneemesha binafsi kimaisha, kwanzia sasa hatakuwa na nafasi na inabidi aondoke katika chama hicho ambacho kazi yake ni kutetea haki za wanyonge.
Komredi Kinana akishangiliwa na wananchi wa Kijiji hicho cha Mtakuja kinachokaliwa na jamii ya wamasai.
 Wananchi wa Kata ya Kia, wakimpatia zawadi ya vazi la Kimasai pamoja na fimbo, Komredi Kinana wakati wa mkutano huo.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutao wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mtakuja, Kata ya Kia, Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Komredi Kinana mjini Hai wakati wa mkutano wa hadhara.
Komredi Kinana akipita kwenye daraja la zamani la Mnepo lililojengwa enzi za ukoloni katika Kijiji cha Kiyungi, mpakani mwa Wilaya za Hai na Moshi Vijijini. Daraja hilo limejengwa kwa waya.
Komredi Kinana akishiriki kupaka rangi aliposhiriki ujunzi wa daraja jipya la Mnepo lililojengwa kwa fedha za Serikali takribani Tshs. bilioni 1 katika Kijiji cha Kiyungi mpakani mwa wilaya za Hai na Moshi Vijijini.
Komredi Kinana akiijaribu mitambo ya Xray iliyopo katika chumba hicho cha upimaji kwa njia ya mionzi.
Nape akipigwa mionzi (Xray) ya mkono wake wa kulia.
Waziri wa Elimu wa zamani, ambaye pia alikuwa waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Israel Nawinga, akimueleza jambo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipotembelewa na viongozi wa CCM kumjulia hali nyumbani kwake Losaa, Masama wilayani Hai jana.

No comments:

Post a Comment