DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, April 17, 2014

WABUNGE WA UPINZANI WASUSIA KIKAO CHA BUNGE MAALUM LA KATIBA JANA

Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana waliondoka kwa hasira katika kikao cha bunge hilo kinachoendelea mjini Dodoma.

SHUGHULI YA UOKOAJI KOREA KUSINI INAENDELEA





Kazi ya uokoaji wa abiria waliokuwa ndani ya feri iliyozama  Korea Kusini jana imeingia siku ya pili. Ambapo maafisa mbalimbali wanaendelea kutafuta takriban abiria 289 waliokuwa ndani ya feri hiyo ambao mpaka sasa hawajulikani walipo. (Hii ni kwa hisani ya BBCswahili)

Wednesday, April 16, 2014

MELI YAZAMA KOREA KUSINI IKIWA NA WATU 460

Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini. Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli hiyo iliyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.

Sunday, April 06, 2014

RC DODOMA: AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA CWT MKOA WA DODOMA


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akiimba wimbo wa mshikamano pamoja na wajumbe wa Baraza la Chama cha Walimu Mkoa wa Dodoma kwenye Mkutano wa chama hicho leo hii.
Wajumbe wa Baraza la Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dodoma
wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma, DR, Rehema Nchimbi (hayupo pichani) wakati wa  Mkutano wa baraza hilo ambapo viongozi hao wameaswa kuongeza  uwazi kwenye mapato na matumizi ya michango ya walimu ili kujipunguzia shutuma kutoka kwa wanachama wao.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na wajumbe
wa Baraza la Chama cha Walimu (CWT) mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kawaida wa chama hicho mapema leo kwenye ofisi za CWT Dodoma.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi, viongozi wa CWT Dodoma na wajumbe wa Baraza la CWT Dodoma muda mfupi mara baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo mapema leo kwenye ofisi za CWT Mkoa.