DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Sunday, April 06, 2014

DODOMA YAADHIMISHA MIAKA 50 YA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA


Watumishi wa maktaba ya mkoa wa Dodoma wakiwa tayari kupokea wananchi wenye mahitaji mbalimbali ya huduma za maktaba kwa ajili ya kuwapa maelekezo ya namna ya kupata taarifa na huduma nyingine hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba, maadhimisho hayo kwa mkoa wa Dodoma yalifanyika viwanja vya maktaba huo.


Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akimsikiliza Mkutubi Msaidizi wa Maktaba ya mkoa wa Dodoma, Ndg. Judith Lugongo wakati anafanya ukaguzi wa maktaba hiyo kukagua vitabu na nyaraka za taarifa mbalimbali kwa ajili ya wasomaji kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba mkoa wa Dodoma hivi karibuni.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akipata ufafanuzi kutoka kwa Mtaalam wa kutafsiri taarifa za vitabu na nyaraka mbalimbali katika lugha za watu wenye mahitaji maalumu/wenye ulemavu wa kuona (nukta nundu), Mwl. Charles Mtimatuku hivi karibuni. Huduma za maktaba nchini zimepiga hatua kiasi cha kuzalisha taarifa na nyaraka mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu.





Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akikagua nyaraka na vitabu mbalimbali alipotembelea mabanda ya maonesho  ya vitabu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba nchini, maadhimisho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya maktaba hiyo hivi karibuni.
Baadhi ya walimu na wanafunzi shule mbalimbali za Dodoma waliojitokeza viwanja vya maktaba ya mkoa Dodoma kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba nchini wakifuatilia salamu za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment