DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, January 28, 2016

YASOMEKAVYO MAGAZETI JANUARI 28, 2016














'NISHA' SASA CHINI YA ULINZI MKALI


Salma Jabu ‘Nisha.
Ili kuhakikisha hasalitiwi katika penzi lake jipya, mkali wa Bongo Fleva Baraka Da Prince, ameajiri baunsa kwa ajili ya kumlinda mpenzi wake Salma Jabu ‘Nisha’ popote anapokwenda.


Kwa mujibu wa Global publisher.co.tz staa huyamefanya hivyo kutokana na wivu uliopitiliza. Nisha alikiri kuwekewa baunsa ambaye ni ndugu wa mpenzi wake, hivyo kila anapokwenda lazima awepo kwa sababu anahofia kusalitiwa.
“Mpenzi wangu Baraka ana wivu sana na ameniwekea baunsa ambaye naenda naye kila sehemu ni mwanaume aliyekamilika, hana upungufu wowote na mimi sijali kuhusu skendo, haziniumizi kwa sababu tunaaminiana, najua hao ni marafiki wa kawaida tu,” alisema Nisha anayetesa na Filamu ya Kiboko Kabisa.

MWANAMITINDO, FLAVIANA MATATA AZINDUA RANGI YA KUCHA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illution  Ltd, Shekha Nasser  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na kushiriki katika uuzaji wa vipodozi vya kucha ambavyo vitakuwa kikiuzwa katika duka lake.
Mwanamitindo wa Tanzania ambaye anafanya kazi za mitindo nchini Marekani, Flaviana Matata amezindua bidhaa za  urembo za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY, amezindua bidhaa hiyo mbele ya waandishi wa habari na kuomba wanawake na watumiaji rangi za kucha  wamuunge mkono kwani ni bidhaa ambayo ipo kwenye soko kwa kipindi hiki kwani kila mwanamke anapenda kupendeza. Kulia ni Afisa mtendaji mkuu wa Shear Illution  Ltd, Shekha Nasser akiwa ni mmoja wa wasambazaji wa  kipodozi cha Kucha ambazo zimezinduliwa jana.
Wakati huhuo amewapongeza wote waliochangia katika kufanikisha yeye kujulikana kimataifa.
Bidhaa za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY  ambazo zimezinduliwa na mwanamitindo Flaviana Matata jijini Dar es Salaam jana.
Bidhaa hizo zitakuwa zikipatikana kwenye maduka mbalimbali na Saluni za Pikasso, Shear Illution  Ltd na Zuri Cosmestics zilizopo jijini Dar es Salam kwa shilingi elfu tano tuu.