DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, January 28, 2016

'NISHA' SASA CHINI YA ULINZI MKALI


Salma Jabu ‘Nisha.
Ili kuhakikisha hasalitiwi katika penzi lake jipya, mkali wa Bongo Fleva Baraka Da Prince, ameajiri baunsa kwa ajili ya kumlinda mpenzi wake Salma Jabu ‘Nisha’ popote anapokwenda.


Kwa mujibu wa Global publisher.co.tz staa huyamefanya hivyo kutokana na wivu uliopitiliza. Nisha alikiri kuwekewa baunsa ambaye ni ndugu wa mpenzi wake, hivyo kila anapokwenda lazima awepo kwa sababu anahofia kusalitiwa.
“Mpenzi wangu Baraka ana wivu sana na ameniwekea baunsa ambaye naenda naye kila sehemu ni mwanaume aliyekamilika, hana upungufu wowote na mimi sijali kuhusu skendo, haziniumizi kwa sababu tunaaminiana, najua hao ni marafiki wa kawaida tu,” alisema Nisha anayetesa na Filamu ya Kiboko Kabisa.

No comments:

Post a Comment