DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, January 06, 2014

SIDO DODOMA YATOA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA NGOZI KWA VIJANA


Mkufunzi wa mafunzo kutoka SIDO  Dodoma Ndg. Shaban Lukandamila akimuonesha Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi mashine ya kutengenezea bidhaa za ngozi iliyotumika wakati wa mafunzo kwa vijana wajasiriamali 27 wa Manispaa ya Dodoma. Mafunzo hayo  yalihitimishwa hivi karibuni na mkuu huyo wa mkoa.

Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza bidhaa za ngozi Ndg.  Shaban  Lukandamila akimuonesha Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi bidhaa za ngozi zilizotengenezwa na vijana wajasiriamali wa Manispaa ya Dodoma waliopatiwa mafunzo ya SIDO Dodoma ya utengenezaji bidhaa za ngozi.



Baadhi ya vijana wajasiriamali kutoka Manispaa ya Dodoma waliohitimu mafunzo ya wiki nne (4) ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi wakisikiliza mawaidha ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (hayupo picha) wakati akifunga mafunzo hayo mapema jana kwenye kituo cha SIDO Dodoma. Mbele  yao ni bidhaa za ngozi walizotengeneza wakati wa mafunzo.
 
Mkuu wa Mkoa Dodoma  Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi cheti kijana mjasiriamali SEIF DAUD aliyehitimu mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi kwenye kituo cha SIDO Dodoma kinachofundisha mafunzo hayo.

Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa tatu kulia waliokaa) na vijana wajasiriamali 27 kutoka Manispaa ya Dodoma waliopata mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi mara baada ya Mkuu wa Mkoa kufunga rasmi mafunzo hayo hivi karibuni  kwenye kituo cha SIDO  Dodoma kinachofundisha utengenezaji wa bidhaa za ngozi. Wengine waliokaa ni viongozi wa SIDO Dodoma na viongozi wa asasi ya marafiki wa elimu Dodoma waliofadhili  mafunzo hayo.


No comments:

Post a Comment