DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, January 15, 2014

ABIRIA WA TRENI YA KATI WAKWAMA MARA MBILI


Abiria waliokwama Mkoani Kigoma tangu Januari 2 na hatimaye juma lililopita kufika Dodoma na kukwama tena baada ya kuharibika kwa njia ya reli eneo la Godegode Mpwapwa wakiwachagua wawakilishi wao  wa kwenda kuzungumza na Mkuu wa Mkoa Dodoma kumweleza adha waliyopata walipokwenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa kwa maandamano, pembeni ni askari wa kulinda ulinzi na usalama.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na abiria wa treni ya kati waliokwama Mkoani Kigoma tangu Januari 2, na kukwama tena Mkoani Dodoma mara baada ya kuwasili Mkoani humo kufuatia uharibifu wa njia ya reli, vilevile mkuu huyo wa mkoa amewaagiza uongozi wa shirika la reli mkoani Dodoma kuwagharamia kwa huduma ya chakula na nyingine muhimu  mpaka watakapoendelea na kumalizia safari yao.


Wawakilishi wa abiria wa treni waliokwama mkoani Dodoma (watatu walioko kulia) walioteuliwa kwenda kuonana na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuelezea adha waliyopata baada ya kukwama kwa safari yao, wakisikiliza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani). Wengine kushoto ni Maafisa wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Wasafiri wawakilishi wa treni ya kati waliokwama Kituo cha Reli Dodoma wakipewa mrejesho  na wenzao juu ya kile walicho kubaliana na Mkuu wa Mkoa Dodoma mara baada ya kumaliza kuzungumza naye ofisini kwake.


No comments:

Post a Comment