Pichani ni basi la abiria lenye namba za usajili T 943 CDH kampuni ya Princes Muro likiteketea kwa moto katika Kijiji cha Ibihwa wilayani Bahi mkoni Dodoma juzi. Kwa mujibu wa maelezo ya Dereva wa basi hilo (jina tunalo) ambalo lilikuwa likisafiri kutoka Shinyanga kuelekea Dar es Salaam, alisema kuwa chanzo cha moto huo ni baada ya gurudumu moja la nyuma kupasuka wakati akifunga breki kwa ajili ya kumshusha abiria aliyekuwa akishuka kijijini hapo. Aidha, abiria wote 59 waliokuwa kwenye basi hilo walitoka salama licha ya baadhi yao kupotelewa na mali zao. |
No comments:
Post a Comment