Rais wa Marekani, Barrack Obama (Pichani) ameliomba Bunge la Congress
kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia
silaha Waasi wa Syria. Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa
japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba
ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo
zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama, hii itakuwa ni mara ya kwanza
kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria,
mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.
Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa Serikali na Wanamgambo wa kundi la waislamu ambao pia wameteka
mpaka ndani ya nchi ya Iraq (ISIS).
|
No comments:
Post a Comment