Mashindano
ya kumsaka Mrembo Kanda ya Mashariki (Redds Miss Eastern Zone 2014)
yatafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nashera, mjini Morogoro.
Mashindano
hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani,
Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro chini ya udhamini wa Redds
Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General
Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon,
Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.
Mratibu
wa masindano hayo, Alex Nikitas aliwataja warembo watakaoshindana siku hiyo
kuwa ni Lucy Julius Diu, Prisca Mengi, Tarchisia Noback Mtui na
Angel Shio ambao wanatoka Morogoro.
Warembo
wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian Andrew na Leila Abdul
Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo kutoka Mtwara ni Nidah Fred
Katunzi, Lightness Mziray na Nelabo Emmanuel.
Pia
warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary
Mpelo na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa warembo hao watakuwa kambini
kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya
mashariki mwaka jana, Diana Laizer.
|
No comments:
Post a Comment