Waziri mkuu wa Ukraine Arseniy
Yatsenyuk
Waziri mkuu wa Ukraine Arseniy
Yatsenyuk amesema kuwa kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia ni uhalifu wa
kimataifa unaopaswa kupelelezwa na mahakama ya jinai iliyoko The Hague.
Waziri huyo mkuu amesema kuwa
mauwaji hayo yametekelezwa na Serikali ya Urusi, huku Rais wa Urusi, Vladimir
Putin, akirushia lawama Ukraine.
Naye Waziri mkuu wa Australia Tony
Abbott amesema kuwa ajali hiyo ya ndege ilionekana kuwa tendo la Ugaidi, kwani
inaonekana ilishambuliwa na waasi wanaofadhiliwa na Urusi.
Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte
amesema nchi yake inaomboleza vifo vya zaidi ya watu 150, raia wa taifa lake
walioangamia katika ajali ya ndege ya Malaysia iliyodunguliwa Nchini Ukraine.
Anasema kuwa kulikuwa na waholanzi
154 kwenye ndege hiyo.
Kati ya walioabiri ndege hiyo,
kulikuwemo takriban watafiti 100 wa ugonjwa wa ukimwi, wafanyikazi katika idara
ya afya na wanaharakati waliokuwa wanasafiri ughaibuni kuhudhuria mkutano wa
kimataifa huko Melbourne.
Aliyekuwa rais wa Jamii ya Kimataifa
inayoshughulikia maswala ya ugonjwa wa Ukimwi, Joep Lange anadhaniwa kuwa mmoja
wa walioabiri ndege hiyo.
|
No comments:
Post a Comment