Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa
ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki
mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na
vikosi vya serikali.
Wanasema abiria wote 298 waliokuwa
katika ndege hiyo ya shirika la Malaysia iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam
kuelekea Kualar Lumpur wamefariki.
Wengi wa abiria hao walikuwa ni raia
wa Uholanzi.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko
alitaja tukio hilo kama kitendo cha ugaidi.
Maafisa wa Ukraine walichapisha kile
walichotaja kuwa mawasiliano ya simu yaliyonaswa kati ya waasi wakiwaeleza
maafisa wa Urusi kwamba ni wao ndio waliohusika katika kuindungua ndege hiyo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
wa Ukraine, Pavlo Klimkin, amesema kuwa serikali ina ushahidi wa kutosha kwamba
ndege hiyo ilidunguliwa.
|
No comments:
Post a Comment