Bibi
Clinton aliingia katika mbio za kuomba kuteuliwa na chama cha Democratic
kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008 lakini alishindwa kwa
Bwana Barack Obama.
Akiwa mgombea anayepewa nafasi na wanachama wa Democratic alitarajiwa kutangaza azma yake ya kugombea miezi kadhaa iliyopita.
Katika video kupitia ukurasa wake wa kampeni, Bibi Clinton alitangaza: "Nagombea urais".
"Wamarekani wamepambana na nyakati ngumu za uchumi," amesema, "lakini hali imebaki kuwanufaisha walio juu.
"Kila siku Wamarekani wanataka kiongozi na nataka kuwa kiongozi," amesema
Bibi Clinton pia alikuwa mke wa rais wakati mumewe Bill Clinton alipokuwa rais wa Marekani. CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment