Phil
Neville akiwa na Ryan Giggs Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya
England na Manchester Utd, Phil Neville amemtetea Yaya Toure wa
Manchester City kwa kusema kuwa mwanandinga huyo si kikwazo kwa klabu
hiyo ya jiji la Manchester kutokana na matokeo mabaya walioyapata katika
mchezo wao wa Jumapili. Neville akizungumza katika mjadala ulifanyika
katika studio za BBC, amesema kuwa kocha Manuel Pellegrini ndiye
aliyekatika wakati mgumu kutokana na kichapo hicho walichokipata kutoka
kwa mahasimu wao wa jiji Manchester Utd, huku akiamini kuwa kocha huyo
ndiye wa kulaumiwa kutokana na maamuzi yake yasiozaa matunda
aliyoyafanya kuelekea katika mchezo huo.
Manchester
City ilibamizwa bao 4-2 na Manchester Utd huku vijana hao wa Etihad
wakifikisha michezo sita kupoteza kati ya michezo nane. CHANZO: BBC |
No comments:
Post a Comment