DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Saturday, October 24, 2015

JK AFUNGUA KITUO CHA MICHEZO KIDONGO CHEKUNDU

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kituo cha michezo cha Jakaya M. Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha michezo  cha Jakaya M. Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada wa klabu ya michezo ya Sunderland ya Uingereza kwa kushirikiana na kampuni ya kufua umeme ya Symbion.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akicheza mpira na baadhi ya watoto wanaopata mafunzo ya michezo katika kituo hicho kinachofunza mpira wa miguu, kikapu na volleyball ya ufukweni.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba mtoto wakati wa Sherehe za ufunguzi wa kituo cha michezo cha Jakaya M. Kikwete Youth park huko kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.





HATIMAYE MAHAKAMA KUU YATEGUA KITENDAWILI CHA MITA WATU KUKAA MITA 200 SIKU YA KUPIGA KURA

Ukiwa bado tuko kwenye masuala ya Uchaguzi Mkuu 2015 habari iliyochukua kasi katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ni kuhusiana na wananchi kusimama mita 200 pale  wanapomaliza kupiga kura siku ya tarehe 25, 2015, sasa mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imesema hairuhusiwi watu kufanya mkusanyiko wowote hata nje ya umbali wa mita 200 baada ya kupiga Kura. Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson alisema…’Ni kwamba kifungu cha 104 kidogo cha kwanza kinakataza  bila kujali umbali wake kutoka kwenye kituo cha kupigia kura ambacho baadae kinabadilika kina kuwa kituo cha kuhesabia kura, na la pili linalokatazwa katika lile jengwa ambapo kura zinahesabiwa mtu haruhusiwi kuvaa nembo au sare ya chama chochote kinachomuonesha yeye yupo upande fulani wa kisiasa’  – Tulia Ackson 

‘Sasa la tatu ambalo pia kile kifungu kinakataza cha 104  kinakataza pia katika umbali wa mita 200 mtu yoyote asivae nembo au kuwa na picha yoyote ya chama au hata bendera yoyote kwenye umbali huo kwa hiyo hayo ndio mambo matatu yaliyokatwaza’ – Tulia Ackson ‘kama mtu hatofuata sheria basi adhabu yake ni Elfu 50 analipa lakini lile limeeleza kuwa ni kosa la jinai  kwahiyo sio tu adhabu ya Elfu 50 mtu atalipa kirahisi hapana lazima akamatwa na kuwa chini ya vyombo vya sheria‘ – Tulia Ackson 
 

Monday, October 19, 2015

PUMZIKA KWA AMANI DEOGRATIAS FILIKUNJOMBE

Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na abiria wengine walipata matatizo ya injini ya chopa namba  5Y-DKK Oktoba 15, 2015  jioni kwenye Hifadhi ya Akiba ya Selous mkoani Morogoro, wakiwa safarini kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Ludewa mkoani Njombe.
Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratias Haule Filikunjombe enzi za uhai wake.
Kept. William Silaa enzi za uhai wake. Kept. Slaa ndiye aliyekuwa rubani wa Helikopta
hiyo yenye namba za usajili 5Y-DKK.

Askari Polisi na Wataalam wakikagua mabaki ya chopa namba  5Y-DKK iliyoanguka Oktoba 15, 2015 jioni ikitokea Dar kuelekea Ludewa sehemu ya Hifadhi ya Wanyama ya Selous ambapo Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe, rubani Kept. William Slaa na abiria wengine wawili - Casablanca Haule na Ngondombwitu Nkwera - walipoteza maisha.

 Timu ya waokoaji wakibeba mabaki ya miili ya marehemu.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea Oktoba 15, 2015 katika Pori la Akiba la Mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. (Picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. (Picha na Freddy Maro)

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika nyumbani kwake Kijichi Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Mjane wa Deo Filikunjombe, Sarah (katikati) akisaidiwa na jamaa zake wakati wa ibada hiyo.
 Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele wakati wa ibada ya kuiombea iliyofanyika nyumbani kwa mbunge huyo Kijichi Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi.
Padri Maxmillian Wambura kutoka Parokia ya Mtakatifu Wote Kiluvya akiyamwagia mafuta ya baraka majeneza hayo.

Waombolezaji wakiwa katika ibada hiyo.
 Familia ya Filikunjombe ikiwa katika ibada hiyo.
Nyumba ya Filikunjombe ambayo inadaiwa amekaa wiki mbili tangu ahamie baada ya kukamilika ujenzi wake.

MAELFU UFILIPINO WAATHIRIWA NA KIMBUNGA KOPPU

Waokoaji nchini Ufilipino wanatatizika kuwaokoa maelfu ya watu wanaokisiwa kuwa wamehamishwa makwao na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo kufuatia kimbunga cha Koppu kilichoikumba tangu hapo jana.
Kimbunga hicho kinachosonga kwa kasi ya chini mno kimesababisha mvua kubwa mno.
Inaripotiwa kuwa maji yamefikia kimo cha mita nne katika sehemu zingine huku kiwango cha mvua kikiendelea kuongezeka.
Maafisa wanasema kwamba watu kadhaa wamekwama juu ya paa za nyumba zao, wakisubiri kuokolewa.
Magari ya kijeshi hayawezi kufikia maeneo hayo, huku kukiwa na upungufu mkubwa wa maboti ya ukoaji.
Maelfu ya watu tayari wamekimbia makwao na kuelekea kwenye maeneo yaliyoinuka na salama.
Hadi kufikia sasa watu 9 wanasemekana kufariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko.
Kimbunga hicho kiitwacho Koppu kimepungua kidogo, lakini kinatabiriwa kuwa kitaendelea kwa siku mbili zijazo.
Mkurugenzi wa shirika la msalaba mwekundu nchini Ufilipino bwana Richard Gordon amesema kuwa tayari wameshatuma maboti ya uokozi ilikuwanusuru wale waliokwama.
Taharuki kubwa imeshuhudiwa kaskazini mwa nchi hiyo, mahala ambapo kimbunga kikali kinapiga kisiwa kikuu cha Luzon, kikiandamana na mvua kubwa. CHANZO: BBCSWAHILI.

KAMATI YA TAIFA STARS YATAMBULISHWA

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Bw. Farough Baghozah leo hii amekutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.

Katika kamati hiyo ya Taifa ya Stars wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu, Wakili Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.

Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:

1. Maandalizi ya timu, zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars
 Mwenyekiti – Imani Madega
 Wajumbe – Msafiri Mgoyi,Teddy Mapunda.

2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo ijayo) na Masoko
 Mwenyekiti – Juma Pinto
 Wajumbe – Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim  Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon,  Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.

 3. Kamati ya Fedha
Mwenyekiti – Farough Baghozah
Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega,          Juma Pinto,        Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.

4. Mikakati ya ushindi – itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.

Pia kamati imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika kuanzia leo hii.  Pia Kamati imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.
Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.

Aidha Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa nyumbani.  Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati Bwana Farough Baghouzah.
 

AU YAUNDA JESHI

Kikosi kipya cha majeshi ya umoja wa Afrika kinafanya mazoeozi yake ya kwanza hii leo nchini Afrika Kusini. 

Mazoezi hayo yanalenga kutathmini utayari wa kikosi hicho kutumika wakati kunapotokea dharura na kunahitajika kikosi cha mbele kitakachodhibiti hali na kuokoa maisha ya watu.
Lakini swali ibuka ni je jeshi hilo litatumwa katika taifa lililochangia wanajeshi wake ?
Mwandishi wa BBC anayeshughulikia maswala ya kiusalama Tomi Oladipo, anasema kuwa madhumuni ya kikosi hicho cha wanajeshi 25,000 kutoka mataifa ya bara Afrika ni kupunguza kutegemea kwa majeshi ya mataifa ya ulaya kuja humu barani kusuluhisha migogoro inayotokea.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza oparesheni yake ya kwanza mwezi januari mwakani.
Hata hivyo umoja wa Afrika unasema unahitajika takriban dola bilioni moja kufadhili shughuli na oparesheni za kikosi hicho.
Mwandishi wa BBC anayeshughulikia maswala ya kiusalama anasema kuwa kuna changamoto za ukosefu wa ushirikiano mwema baina ya mataifa shirika.
Cameroon imejitolea kuwa mwenyeji wa kikosi hicho ikisema watakita kambi yao katika mji wa Douala. 
 
Vilevile anasema kuwa mataifa mengi hayajajitolea kuunga mkono jeshi hilo kisiasa.
Jeshi hilo linatarajiwa kuwa na vikosi vitano.
Kwa sasa Cameroon imejitolea kuwa mwenyeji wa kikosi hicho ikisema watakita kambi yao katika mji wa Douala. CHANZO: BBCSWAHILI