Waokoaji nchini Ufilipino
wanatatizika kuwaokoa maelfu ya watu wanaokisiwa kuwa wamehamishwa
makwao na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo kufuatia kimbunga
cha Koppu kilichoikumba tangu hapo jana.
Kimbunga hicho kinachosonga kwa kasi ya chini mno kimesababisha mvua kubwa mno.
Inaripotiwa kuwa maji yamefikia kimo cha mita nne katika sehemu zingine huku kiwango cha mvua kikiendelea kuongezeka.
Maafisa wanasema kwamba watu kadhaa wamekwama juu ya paa za nyumba zao, wakisubiri kuokolewa.
Magari ya kijeshi hayawezi kufikia maeneo hayo, huku kukiwa na upungufu mkubwa wa maboti ya ukoaji. |
No comments:
Post a Comment