Ukiwa bado tuko kwenye masuala ya Uchaguzi Mkuu 2015 habari iliyochukua kasi
katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ni kuhusiana na wananchi
kusimama mita 200 pale wanapomaliza kupiga kura siku ya tarehe 25,
2015, sasa mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imesema hairuhusiwi watu kufanya mkusanyiko
wowote hata nje ya umbali wa mita 200 baada ya kupiga Kura. Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson alisema…’Ni
kwamba kifungu cha 104 kidogo cha kwanza kinakataza bila kujali umbali
wake kutoka kwenye kituo cha kupigia kura ambacho baadae kinabadilika
kina kuwa kituo cha kuhesabia kura, na la pili linalokatazwa katika lile
jengwa ambapo kura zinahesabiwa mtu haruhusiwi kuvaa nembo au sare ya
chama chochote kinachomuonesha yeye yupo upande fulani wa kisiasa’ – Tulia Ackson | |
No comments:
Post a Comment