DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, February 17, 2014

RC DODOMA ATEMBELEA KIKUNDI CHA NGOMA KILICHOANZISHWA NA JKT MAKUTUPORA

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipanda mti wa mzabibu kwenye eneo la kambi ya jeshi Makutupora kama ishara ya kumbukumbu alipotembelea kambini hapo jana kujionea shughuli za sanaa ya ngoma kutoka kwa kikundi kipya cha sanaa za ngoma cha JKT Makutupora.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi (kushoto) akiongozana na kamanda wa kikosi 834 KJ  Makutupora Luteni Kanali Fume (katikati) na  Kaimu Mkuu wa shule ya kijeshi Makutupora Meja Ruwa (kulia) wakielekea bwalo la jeshi kambini hapo kukagua shughuli za sanaa za kikundi kipya cha sanaa ya ngoma cha JKT Makutupora hivi karibuni.

Kikundi kipya cha sanaa ya ngoma za asili cha JKT Makutupora Dodoma kikitumbuiza nyimbo ya asili ya wenyeji wa mtwara mbele ya Mkuu wa Mkoa Dodoma (hayupo pichani) hivi karibuni wakati mkuu huyo wa mkoa alipofika kambini hapo kukagua shughuli za kikundi hiko kipya.

No comments:

Post a Comment