TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasheherekea maadhimisho
ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku yakiwemo mafanikio makubwa dhahiri na
ya kujivunia katika sekta ya mawasiliano nchini.
TCRA ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2003
ili kusimamia Sekta ya Posta na Mawasiliano ya Elektroniki ikiwemo simu,
utangazaji, wavuti pamoja na huduma za Posta. TCRA ilkianzishwa kwa Sheria Na.
12 ya mwaka 2003 iliyoziunganisha Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya
Utangazaji Tanzania (TBC).
Mkakati mahususi wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania ni “Kuboresha Maisha ya Watanzania kupitia mfumo makini na thabiti ili
kuhakikisha kunakuwa na huduma za mawasiliano kwa wote nchini”.
Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Tanzania imeshuhudia kukua kwa kasi
kwa Sekta ya Mawasiliano. Mamlaka ilianzisha mfumo wa leseni za Muingiliano
mnamo tarehe 23 Februari 20005.
Mfumo huu wa leseni za muingiliano
(Convergence Lisensing Framework) umekuwa chachu ya kuongezeka kwa miundombinu
mbalimbali ya mawasiliano, huduma mbalimbali kwa kutumia mtandao wa mawasiliano
ikiwemo wavuti (internet) na utangazaji.
Makampuni ya simu yameongezeka kutoka
kampuni moja ya simu TCRA ilivyoanzishwa mwaka 2003 hadi kufikia makampuni saba
(7) yenye wateja wenye laini za simu takribani milioni 28 kulinganisha na idadi
iliyokuwepo miaka kumi iliyopita. Huduma za simu za mkononi zimebadilisha
maisha ya Watanzania kutokana na huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia simu
za mkononi.
Kuanzia huduma za kutuma fedha kupitia
simu, malipo ya Ankara mbalimbali na huduma nyingine nyingi zilizobadilisha
maisha na uchumi wa wananchi wa taifa hili.
Sekta ndogo ya Posta nayo haijabaki nyuma
kwani kumekuwepo na ongezeko la watoa huduma kutoka mmoja hadi zaidi ya hamsini
wenye kutoa hduma ndani nan je ya Tanzania. Tunatarajia mabadilikjo makubwa kwa
watanzania hasa baada yan kukamilika kwa mradi wa anwani mpya za makazi na
misimbo ya Posta.
Hali kadhalika, yako mabadiliko makubwa
sana katika msekta ndogo ya utangazaji. Kutoka nchi yetu kuwa na Radio moja
hadi Zaidi ya redio 85. Aidha kutokuwepo kwa Kituo cha Utangazaji wa Runinga
hadi vituo vya utangazaji vipatavyo 26. Watumiaji wa wavuti (intanet
wameongezeka kutoka watumiaji million moja hadi takribani milioni 8 na ushee.
Sekta ya Mawasiliano imekuwa chimbuko la maendeleo ya nchi kwa kutoa ajira kwa
watanzania wengi na hali kadhalika kuongeza mapata ya serekali kwa tozo na kodi
mbalimbali zinazotolewa katika sekta.
Mamlaka ya Mawasiliano imeshinda tuzo
mbalimbali katika masuala ya Udhibiti na Usimamizi Bora wa Huduma za
mawasiliano nchini katika kipindi cha kuweko kwake miaka kumi iliyopita. Nchi
mbalimbali zimekuja Tanzania kujifunza udhibiti na usumamizi wa masuala nyeti ya
mawasiliano kama vile masuala ya uhamaji kuelekea mfumo mpya wa utangazaji wa
dijitali, Mifumo ya uanzishwaji wa anwani za makazi na misimbo ya posta,
Usimamizi mzuri wa masafa na namba za mawasiliano na mambo mengine mengi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO
TANGU 25 – 29 NOVEMBA 2013
Katika kusheherekea miaka kumi ya Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania, kutakuwa na maadhimisho ya wiki nzima yenye matukio
mbalimbali. Tukianzia na mkutano huu na waandishi wa habari uliokusudia kutoa
taarifa kwenu na kwa wananchi kuhusu maadhimisho haya, kutakuwa na matukio
kadha wa kadha kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho yanayotarajiwa
kufanyika tarehe 29 Novemba 2013.
Maadhimisho haya yanafanika chini ya kauli
mbiu ya; Miaka 10 ya TCRA: Miaka Kumi ya Mapinduzi Katika Sekta ya Mawasiliano
Kesho tarehe 26 Novemba 2013 kutakuwa na
tukio maalumu kwa wafanyakazi wa mamlaka ambapo wale waliokuwepo tangu wakati
wa kuanzishwa kwa TCRA watatunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali kutambua
mchango wao kwa taasisi.
Aidha siku ya tarehe 27Novemba 2013;
kutakua na sherehe ya kutoa udhamini kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya
juu wanaochukua masomo ya mawasiliano, sayansi na teknolojia. TCRA kwa kipindi
cha miaka miwili mfululizo imekuwa ikitoa udhaminim katika masomo hayo kwa
wanafunzi mahiri kwa nia ya kukuza weledi na kuboresha utumishi katika sekta ya
mawasiliano chini ya kinachoitwa “TCRA ICT SCHOLARSHIPS” kwa wanafunzi wa
digrii ya kwanza, digrii za Uzamili na Uzamivu.
Kuanzia tarehe 27 – 29 Novemba, kutakuwa
na maonesho maalumu katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa Mlimani City
ambapo watoa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini wataonesha mafanikio yao
na huduma wanazotoa kwa wananchi. Napenda kuchukua fursa hii kuwasihi waandishi
wa habari kuhudhuria maonesho haya ili kujifunza na kutumia fursa hiyo
kuelimisha jamii ya watanzania kuhusu huduma mbalimbali za mawasiliano
zinazopatikana nchini ili wachangamkie fursa.
Hali kadhalika, katika maadhimisho haya,
TCRA imeandaa washa maalumu ya siku mbili wa wadau wa mawasiliano kujadili
fursa, changamoto pamoja na namna gani kwa pamoja tunavyoweza kufanya
mawasiliano kuwa bora Zaidi nchini mwetu.
Warsha hiyo itafanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mlimani City na itafunguliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na Mhe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utaendelea hadi tarehe 29
Novemba 2013. The Opening Ceremony will be graced by Dk. Mohammed Gharib
Billal.
Wadau mbalimbali wa Mawasiliano kama vile
kituo cha Habari cha Tanzania Network Information Centre (tzNIC), Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote – Universal Communications Services Access Fund (UCSAF),
Wamiliki wa Vyombo Vya Habari – Media Owners Association of Tanzania (MoAT-
Broadcasting), na Umoja wa Makampuni ya Simu – Mobile Operators Association of
Tanzania (MoAT-Mobile Telephony Companies), Africa Media Group, Agape
Associates and TTCL watawasilisha mada mbalimbali.
Vyombo vya Habari vinakaribishwa katika
shughuli zote za maadhimisho ya Miaka 10 ya TCRA ili kutoa elimu kwa umma
lakini pia kama fursa ya kujionea mafanikio ya sekta ya mawasiliano katika
kipindi cha miaka kumi iliyopita ili kuwawezesha wananchi kufahamu tulikotoka,
tunakoenda na fursa zilizoko katika sekta ili kuboresha maisha yao.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
25th November
2013