DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, November 13, 2013

JE, WAJUA? JIFUNZE ASILI YA JINA LA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI...!

Nadhani Kibao kinajieleza...

Sehemu ya uwanda unaovutia katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi iliyopo Mkoani Katavi.

Baadhi ya wanyama wakiwa malishoni hifadhini humo...

Kiboko wa Katavi huyo...na hapa ni katika mwambao wa Ziwa Iku (halipo pichani).

Hapo sasa...nani zaidi?

Tazama wanavyovutia na kupendeza...tuwalinde na kuwatunza kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo...!

Watanzania wenzangu tutunze rasimali za nchi yetu... Kwa pamoja tunaweza!

Jamani tuwapende watoto! Mzee wa Dom Land nilipata kuwa huko hivi karibuni...nilitembelea hifadhi hiyo kiukweli nadiliki kusema ndiyo hifadhi pekee nchini ambayo ina mandhari ya kuvutia na inaleta hamasa unapofanya utalii. Watanzania tujenge utamaduni wa kufanya utalii wa ndani na familia zetu kuna mengi ya kujifunza .

Mzee wa Dom Land nikivuta pumzi kidogo baada ya heka heka za hifadhini humo. Kulia kwangu ni Bw. Emmason Emma Kawa, Kaimu Afisa Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi anaefuata ni dereva Mood.

Oohoooo...! Baadaye ikawa hivi...si jambo la kushangaza sana kutokea katika hifadhi hiyo kwani eneo kubwa ni ardhi oevu.

No comments:

Post a Comment