DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, November 14, 2013

DUWASA YAJIPANGA KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KWA WADAU WAKE


Kazi ya ulazaji wa mabomba ya majisafi-UDOM ikiendelea.

Tenki la maji lenye ujazo wa 3000 M3 limejengwa UDOM 
Slabs zilizojengwa katika maeneo ya mabwawa-UDOM

Ulazaji wa slabs kwenye mabwawa ya kutibu majitaka -UDOM

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi katika utoaji wa huduma ya majisafi na uondoshaji majitaka mjini Dodoma hasa ile ya uwezo mdogo wa kuzalisha maji na kuyasambaza  katika maeneo mengi yaliyopimwa, kwa sasa Mamlaka hiyo kupitia mpango wake wa muda mfupi na wa kati inatekeleza Mradi wenye lengo la kuboresha huduma ya majisafi mjini Dodoma kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Eng. Peter A. Mokiwa alieyoituma kwenye vyombo vya habari leo, Eng. Mokiwa alitaja miradi hiyo kuwa ni ule majisafi na majitaka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)na mradi wa chanzo mbadala cha Majisafi Farkwa.
Pamoja na miradi hiyo Eng. Mokiwa aliitaja baadhi ya miradi inayosimamiwa na DUWASA kwa niaba ya Wizara ya Maji kuwa ni Ujenzi wa Jengo la ofisi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi   wa Mazingira Mpwapwa
Mradi wa Uboreshaji wa huduma ya Maji Mamlaka ya   Majisafi na Usafi wa Mazingira Kibaigwa

No comments:

Post a Comment