DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, November 21, 2013

RC DODOMA AZINDUA RASMI MSIMU WA KILIMO 2013


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akiwapungia mkono wananchi na wadau wa kilimo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa msimu wa kilimo kwa mwaka 2013 kimkoa ambapo ulifanyika hivi karibuni katika Skimu ya Mpunga ya Matajila Wilayani Bahi, Dodoma. Trekta linaloonekana ni moja ya matrekta ya kisasa yanayomilikiwa na Mwekezaji Field Masters Ltd anayeendesha kilimo kwa njia Carbon Farming Conservation Agriculture na ni moja ya zana bora na za kisasa za kilimo zitakazotumika katika msimu huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (aliyevaa kilemba cha rangi ya pinki) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2013 huku akishuhudiwa na wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akisaidiwa kushuka kwenye trekta na Mkurugenzi wa Kampuni ya Field Masters Ltd Bw. Mick Dennis mara baada ya kufanya uzinduzi wa msimu wa kilimo 2013. Uzinduzi huo ulitanguliwa na tathmini ya msimu uliopita wa mwaka 2012. 

Pichani ni trekta lililonunuliwa na mfugaji Nzije Shanga wa Kijiji cha Mkakatika wilayani Bahi, Dodoma ambaye amehamasishwa kuvuna mifugo yake na kuwekeza katika sekta ya kilimo. Mfugaji huyo alikabidhiwa trekta hilo siku ya uzinduzi wa msimu wa kilimo 2013 (tarehe 15/11/2013) kijijini hapo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi. (wote hawapo pichani).

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikatika aliyevaa kilemba na miwani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafamilia ya Mzee Nzije Shanga (anayefuata kushoto kwa Mkuu wa Mkoa). Mzee Shanga ni moja ya wafugaji maarufu wilayani Bahi waliohamasika kuvuna mifugo yao na kuwekeza katika sekta nyingine za kiuchumi.    

No comments:

Post a Comment