|
Naibu
Waziri wa Maji Mhandisi Benelith Mahenge (katikati) akitoa maagizo juu ya
miradi ya maji kwa wakurugenzi na Wahandisi wa Maji wa wilaya za Mkoa wa Dodoma
wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Naibu Waziri huyo aliyoifanya wiki
zima alipotembelea miradi ya maji mkoa wa dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dr. Rehema Nchimbi na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe.
Jumanne Ngede.
|
|
Wadau
na viongozi wnaosimamiasekta ya maji Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu waziri
wa Maji akitoa majumuisho ya ziara aliyoifanya wiki zimakukagua
utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Dodoma.
|
|
Baadhi
ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Dodoma
wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maji (hayupo pichani) wakati wa majumuisho ya
ziara aliyoifanya mkoani humo kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mpwapwa Bi. Mwajina Lipinga, Mkurugenzi wa Bahi
Bi. Rachel Chuwa na Mkurugenzi wa Kongwa Bi. Bibie Mnyamagoha.
|
............................................................
Naibu
waziri wa Maji Mhandisi Benelith Mahenge (Mb) mnamo tarehe 12 Novemba
hadi 16 Novemba 2013 alifanya ziara mkoani Dodoma na kutembelea miradi ya maji
inayotekelezwa kwenye wilaya za mkoa wa Dodoma na Mamlaka ya majisafi na usafi
wa mazingira mjini Dodomaa -DUWASA. Alasiri ya Jumamosi Novemba 16,
alikutana na Viongozi wa Mkoa na Watendaji/wataalamu wanaosimamia Sekta ya maji
mkoani Dodoma kwa ajili ya majumuisho ya ziara nzima. Mkutano huo wa Majumuisho
ulifanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Dodoma.
No comments:
Post a Comment