DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, November 05, 2013

RC DODOMA AKABIDHI MATREKTA YA MKOPO KWA WAKULIMA MKOANI DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa tatu kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa matrekta ya mkopo  kwa wakulima kutoka wilaya za mkoa wa Dodoma, hafla hiyo ilifanyika jana kwenye ofisi za Kampuni ya NAM Ltd mjini Dodoma ambayo inakopesha matrekta hayo kwa wakulima, jumla ya matrekta matano yenye  thamani ya shilingi 175,000,000.00  yalikopeshwa kwa wakulima.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akimkabidhi ufunguo ya trekta mkulima Kalanga Ngudong' wakati wa hafla ya kukabidhi kwa wakulima matrekta hayo ya mkopo yaliyotolewa na kampuni ya kusambaza matrekta ya NAM Ltd ya Mjini Dodoma, anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa NAM Ltd Bw. Aspenas Mwaranga, hafla hiyo ilifanyika jana mjini Dodoma.

Mkulima Kalanga Ngudong' kutoka Kijiji cha Magungu Chamwino Dodoma akiwasha trekta lake alilokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani) baada ya mkulima huyo kupata mkopo wa trekta hilo kutoka kampuni ya NAM Ltd ya mjini Dodoma inayokopesha matrekta hayo (NAM Truck), hafla hiyo ya kukabidhi matrekta ilifanyika jana kwenye viwanja vya kampuni ya NAM mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment