DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, December 24, 2013

VODACOM YAKABIDHI MSAADA WA KOMPYUTA 3 NA RUTA MOJA KWA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA DODOMA


Mkuu wa Wilaya Chamwino Fatma Ally (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma-CPC, Joyce Kasiki (kulia)  Kompyuta zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom ikiwa ni msaada kwa chama hicho ili kusaidia shughuli zao za uandishi wa habari, anayeshuhudia (katikati) ni mwakilishi wa Vodacom Salum Mwalimu. Hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 5 ilifanyika kwenye ofisi za chama hicho jana.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Ally akiongea na Waandishi wa habari wa Dodoma kuhusu kuboresha utendaji wao wa kazi, kufanya tafiti za mtandaoni na kutoa habari na taarifa zenye ubora na uhakika wa hali ya juu kwa kutumia Kompyuta hizo. 
Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom, Salum Mwalimu akielezea azma ya Vodacom kusaidia vyama vya waandishi wa habari vya mikoa ili kusaidia kunyanyua ubora wa shughuli za uandishi wa habari nchini. Jumla ya Kompyuta 3 na Ruta 1 ya kuunganisha mtandao (vyenye shaman ya zaidi ya milioni 5) vimetolewa na Vodacom kwa waandishi hao jana.

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Ally (wapili kushoto waliokaa), kulia kwake ni mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalimu pamoja na waandishi wa habari mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya kampuni hiyo kukabidhi msaada wa Kompyuta 3 na ruta 1 kwa Chama cha Waandishi wa Habari nkoa wa Dodoma jana.



Tuesday, December 17, 2013

KATIKA PITA PITA VIJIJINI MWISHONI MWA JUMA LILILOPITA...

"Ngombe hazeeki maini...!" Walipata kunena wahenga...nami leo nimeshuhudia katika Kijiji cha Mkakatika Wilayani Bahi.

Ama kweli ufugaji kazi...hapa ni sehemu ya kuhifadhia ndama ambao umri wa kwenda machungani bado. Ndama hao wapatao mia niliwakuta kwa Mfugaji Nzije Shanga ambaye uongozi wa Wilaya ya Bahi umemhamasisha kuvuna mifugo yake ili aboreshe maisha yake kwa kuwekeza katika sekta nyingine za kiuchumi. Na katika hilo ameitikia kwa kasi kubwa.

Wakinamama wa mjini mpo! Maana nyiye yenu gesi... Pichani ni Bi. Gaudensia Nzije akiwa kwenye chumba anachotumia kuhifadhia kuni kwa ajili ya matumizi katika msimu wa masika. kwani wakati wa msimo huo upatikanaji wa nishati hiyo ni mgumu.


Ama kweli "Ukistaajabu ya Musa...najua utamalizia!" Nimeikuta Kijiji cha Mkakatika studio hiyo (PAMOJA RECORD'S). Kaka yangu MASTER J upooo? 

MASHINDANO YA MICHEZO YA VYUO VIKUU TANZANIA 2013


Wanafunzi wachezaji kutoka vyuo vikuu 16 nchini wakipita kwa maandamano mbele ya jukwaa kuu,  wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu Tanzania yaliyoanza Desemba 12 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Sehemu ya Wanamichezo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakishangilia ufunguzi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu Tanzania yaliyoanza Desemba 12 mjini Dodoma, michezo hiyo inaandaliwa na Jumuiya/Taasisi ya Michezo ya Vyuo Vikuu Tanzania (TUSA ), jumla ya vyuo vikuu 16 nchini vinashiriki mashindano hayo.

Sehemu ya Wanamichezo kutoka vyuo vikuu hapa nchini wakishangilia ufunguzi wa mashindano ya vyuo vikuu Tanzania yaliyoanza Desemba  12 mjini Dodoma.

Wanamichezo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiserebuka kwaito kushangilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani) mara baada ya kufungua mashindano ya Wanamichezo ya vyuo vikuu nchini yaliyoanza Desemba 12 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Vyuo vikuu 2013 nchini ambapo amewataka wasomi kutambua kuwa kwa sasa michezo ni moja ya sekta zinazoongoza kwa kuingiza kipato na utajiri kitaifa na kimataifa, vilevile aliwataka wanachuo hao kuitumia michezo kujenga ushirikiano na kudumisha amani na utulivu.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua na kusalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya wanaume ya Chuo Kikuu cha Elimu Zanzibar wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu dhidi ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwaasa Wanamichezo kuzingatia kanuni za michezo, ushirikiano na utulivu kwenye michezo wakati wa mechi ya ufunguzi ya mpira wa miguu iliyowakutanisha Chuo Kikuu cha DSM na Chuo Kikuu cha Elimu Zanzibar.

Monday, December 09, 2013

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU MKWAWA CHAENDESHA MAHAFALI YA TANO MJINI IRINGA...

Brass Bandi ya Jeshi la Magereza Kiwila wakiongoza maandamano ya viongozi waandamizi katika Mahafali ya Chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa manispaa ya Iringa.

Mkuu wa chuo Pr. Amandina Lihamba akihutubia wahitimu katika Mahafali ya Tano 7- Des-2013 yaliofanyika viwanja vya michezo chuoni Mkwawa manispaa ya Iringa.

Muhitimu Mbuba Veronica akitoa mkono kwa viongozi baaba ya kusoma na kukabidhi risala kwa mgeni rasimi katika Mahafali chuoni Mkwawa.

Mhe. Balozi Nicholaus Kuhanga Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mgeni rasmi katika mahafali ya tano ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa akiwahudhurisha wanafunzi waliofuzu na kustahili kupata Shahada (DIGRII) za Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Jumla ya wanafunzi (591) wamestahili kupata Shahada ya Elimu ya Jamii na Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kupitia Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa. Picha zote kwa hisani ya Mjengwablog.

"UHURU NI KAZI"...RC DODOMA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA KWA MTINDO WA AINA YAKE....


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba cha kijani) akimsikiliza kwa makini kupata utangulizi Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Betty Mkwasa (katikati) mara baada ya kuwasili katika eneo lenye ukubwa wa ekari 50 lililotengwa maalum na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa ajili ya Chama cha Ushirika wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma. Eneo hilo ndipo yalipofanyika maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika kimkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akiendesha harambee kwa Wakuu wa Idara kuchangia fedha kwa ajili ya kusafishia shamba la ekari 50 la
Chama cha Ushirika wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma ili waweze kulima msimu huu wa kilimo. Aliyemshika mkono ni Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Ndg. Mohamed Mkwawa. Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 1.6 zilipatikana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akipokea mkono wa shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma, Ndg. Anyelwisye Jonas mara baada ya kukabidhi shilingi laki moja aliyowaahidi vijana hao siku ya uzinduzi wa msimu wa kilimo mwezi uliopita. Aidha, katika harambee aliyoiendesha alichangia tena shilingi laki mbili. Anayeshuhudia kwa kupiga makofi katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Betty Mkwasa.




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akimshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Ndg. Rechal Chuwa (mwenye flana nyeupe) kuwa ahakikishe vijana hao wanajengewa kibanda katika eneo la shamba hilo kwa ajili ya mlinzi atakayeajiriwa na vijana hao kutunza shamba hilo. Pia, alimuagiza  kuwa katika mipango ya Halmashauri ya kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji wilayani hapo ahakikishe kwamba vijana hao wanapatiwa maji ili waendeshe kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kuliko cha sasa ambacho ni cha kutegemea mvua.




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) katika picha zote tatu, akiwakabidhi vijana vinywaji aina ya juisi ikiwa ni kuwawezesha ili waweze kujituma na kufanya kazi kwa bidii wakati wa kusafisha shamba lao.






Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akishirikiana na vijana wa Chama cha Ushirika wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma kusafisha shamba lenye ukubwa wa ekari 50 walilotengewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi katika Kijiji cha Mkakatika wilayani humo ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliosimama mwenye kilemba cha kijani) akiwa katika picha ya pamoja na vijana mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika ambayo kimkoa yamefanyika leo wilayani Bahi.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliosimama mwenye kilemba cha kijani) akiwa katika picha ya pamoja na vijana mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika ambayo kimkoa yamefanyika leo wilayani Bahi.
 
 ..........................................................

 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi amewaasa vijana nchini kuacha kutumiwa kama daraja na baadhi ya viongozi au vyama vya siasa kwa ajili ya manufaa yao, bali amewataka wazitumia fursa na rasilimali zilizopo kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Dr. Chimbi ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo kimkoa yalifanyika wilayani Bahi katika Kijiji cha Mkakatika ambako jumla ya vijana hamsini (50) wa Chama cha Ushirika wa Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko walikutana kwa lengo la kusafisha eneo lenye ukubwa wa ekari 50 walilotengewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa ajili ya Kilimo ikiwa ni jitihada za serikali kuwawezesha vijana kujiajiri.

"Vijana kwa sasa ni wakati wa ninyi kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko maslahi yenu binafsi...hivyo kupitia kilimo mtakachoendesha katika eneo hili, ni matumaini yangu kuwa kwa faida mtakayopata mtakuwa chachu ya maendeleo na mabadiliko kwa vijana wengine nchini". Alisema Dr. Nchimbi.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha kuwa maadhimisho ya sherehe za kitaifa kama hizo kutofanyika majukwaani kwa viongozi kushuhudia ngoma na burudani nyingine wakati ni muda wa kutekeleza MATOKEO MAKUBWA SASA, badala yake wawaongoze vijana katika fursa na rasilimali zilizopo na namna zitakavyowakwamua kiuchumi. Ambapo kwa kufanya hivyo, vijana wataendelea kuuenzi uhuru huo kwa vitendo.  

Pamoja na hayo, Dr. Chimbi aliendesha harambee kwa viongozi mbalimbali waliofika katika maadhimisho hayo kwa ajili ya kuchangia fedha za kuwasaidia vijana hao kusafishia shamba hilo, ambapo zilipatikana shilingi 1,650,000.00.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ilikuwa ni "Vijana ni nguzo ya rasilimali watu, tuwaamini na tuwatumie kwa manufaa ya taifa letu"