.......................................................................
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.
Rehema Nchimbi ameelezea kutokuridhika na kasi iliyopo sasa katika kupunguza
maambukizi mapya, vifo na unyanyapaa vitokanavyo na UKIMWI.
Dr. nchimbi alisema takwimu
zinaonesha kushuka kwa tatizo la maambukizi lakini linashuka kwa kasi ndogo na
kubainisha kuwa umefika muda wa kuweka bidii kubwa zaidi na mbinu kabambe ili
kufikia lengo la kitaifa la kuzuia maambukizi mapya, vifo na unyanyapaa
vitokanavyo na UKIMWI hadi kufikia kiwango cha sifuri tatu ifikapo 2015.
Hayo aliyasema jana
alipokuwa akihutubia wananchi wa mkoa wa Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku
ya UKIMWI duniani ambayo kimkoa Dodoma yalifanyika katika kijiji cha Dabalo
Chamwino.
Ili kufanikisha lengo la
kitaifa, Dr. nchimbi aliwaagiza wakuu wa Wilaya na watendaji ngazi mbalimbali
mkoani Dodoma kuhakikisha pamoja na kuwepo kwa mkakati wa kitaifa, wanaweka
mikakati na mbinu ndogo za kuhakikisha wanazuia tatizo hili kwwenye maeneo yao
na kutolea mfano wa sheria ndogo zilizoundwa kwenye ngazi za msingi za mamalaka
ya serikali za mitaa na kuweka agenda kwenye mikutano.
Vilevile ili kupunguza
tatizo la unyanyapaa katika Mkoa wa Dodoma na wagonjwa kujificha, Dr. nchimbi
amewaagiza viongozi na watendaji ngazi mbalimbali kuhakikiosha wanazingatia na
kuwapa haki zao za msingi wale wote wanaoishi na VVU/UKIMWI mahala popote iwe
kwenye masuala ya kijamii, kisheria, ardhi, ajira, watoto wanaoishi na
VVU/UKIMWi kupatiwa elimu bila ubaguzi na pia kushirikishwa kwenye maamuzi.
Dr. nchimbi amesema haitoshi
kusema tunaondoa unyanyapaa wakati wananchi hawaoni uzito na utekelezaji wa
azimio hili kwa vitendo, pia ametaka wilaya kuweka mkakati wa makusudi wa
kuwalinda watoto hasa wa kike dhidi ya kufanyiwa vitendo hatarishi vinavyoweza
kuwasababishia maambukizi ya UKIMWI kama vile ubakaji na unyanyasaji.
Akitoa ushuhuda wake Bi.
Hawa Ramadhani mkazi wa kijiji cha Msanga Chamwino amesema yeye anaishi na Virusi vya UKIMWI kwa miaka kumi (10) sasa tangu alipogundulika mwaka 2004 na
kuwa hadi leo anaishi na kuendesha maisha yake kupitia kilimo.
Bi. Hawa anasema anafuata
masharti na ushauri wa wataalamu wa Afya, ameshauri ili kuzuia unyanyapaa ipo
haja ya kila mtu katika jamii kuwa wazi hassa pale mtu abnapokutwa na Virusi .
Bi Hawa anasema unapokuwa wazi jamii itakuelewa, itakuheshimu na itakufuata
haitakuacha pekeako.
Kwa upande wake Afisa
Maendeleo Mkoa wa Dodoma Bi. Happiness Huiza alibainisha kuwa Mkoa wa Dodoma
umefanikiwa kupunguza ushamiri wa VVU kutoka 4.9% mwaka 2003/4 hadi
kufikia 2.9 mwaka 2012/13. Vilevile hadi
kufikia Disemba 2012 Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kuandikisha jumla ya watu 28,
219 ambapo wanaotumia dawa ARVs kufubaza makali ya UKIMWI ni 16,413.
Bi. Hiza ameongeza kuwa Mkoa una vituo 340 vinavyotoa huduma
za upimaji na tiba na kwa kipindi cha mwaka 2012/13 jumla ya akinamama
wajawazito 55,484 walishauriwa kupima VVU kati yao 1,183 walikutwa na
maambukizi ambapo kati ya watoto 632 waliozaliwa na akinamama wenye VVU ni
watoto 96 pekee ndio walipata maambakuzi kutoka kwa mama zao lakini waliobakia
wote walisaidiwa kitaalamu wakazaliwa salama.
No comments:
Post a Comment