|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba cha kijani) akimsikiliza kwa makini kupata utangulizi Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Betty Mkwasa (katikati) mara baada ya kuwasili katika eneo lenye ukubwa wa ekari 50 lililotengwa maalum na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa ajili ya Chama cha Ushirika wa
Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma. Eneo hilo ndipo yalipofanyika maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika kimkoa.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akiendesha harambee kwa Wakuu wa Idara kuchangia fedha kwa ajili ya kusafishia shamba la ekari 50 la Chama
cha Ushirika wa
Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma ili waweze kulima
msimu huu wa kilimo. Aliyemshika mkono ni Mweka hazina wa Halmashauri
ya Wilaya ya Bahi, Ndg. Mohamed Mkwawa. Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 1.6 zilipatikana. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akipokea mkono wa shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa
Chama cha Ushirika wa
Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma, Ndg. Anyelwisye
Jonas mara baada ya kukabidhi shilingi laki moja aliyowaahidi vijana hao
siku ya uzinduzi wa msimu wa kilimo mwezi uliopita. Aidha, katika harambee aliyoiendesha alichangia tena shilingi laki mbili. Anayeshuhudia kwa kupiga makofi katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Betty Mkwasa. |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akimshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Ndg. Rechal Chuwa (mwenye flana nyeupe) kuwa ahakikishe vijana hao wanajengewa kibanda katika eneo la shamba hilo kwa ajili ya mlinzi atakayeajiriwa na vijana hao kutunza shamba hilo. Pia, alimuagiza kuwa katika mipango ya Halmashauri ya kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji wilayani hapo
ahakikishe kwamba vijana hao wanapatiwa maji ili waendeshe kilimo cha
kisasa cha umwagiliaji kuliko cha sasa ambacho ni cha kutegemea mvua.
|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (kulia) katika picha zote tatu, akiwakabidhi vijana vinywaji aina ya juisi ikiwa ni kuwawezesha ili waweze kujituma na kufanya kazi kwa bidii wakati wa kusafisha shamba lao. |
|
Pichani
ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akishirikiana na vijana
wa Chama cha Ushirika wa
Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko mkoani Dodoma kusafisha shamba
lenye ukubwa wa ekari 50 walilotengewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
katika Kijiji cha Mkakatika wilayani humo ikiwa sehemu ya maadhimisho ya
miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika. |
|
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliosimama mwenye kilemba cha kijani) akiwa katika picha ya pamoja na vijana mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika ambayo kimkoa yamefanyika leo wilayani Bahi. |
|
Pichani
ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliosimama
mwenye kilemba cha kijani) akiwa katika picha ya pamoja na vijana
mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika
ambayo kimkoa yamefanyika leo wilayani Bahi. |
..........................................................
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi amewaasa vijana nchini kuacha
kutumiwa kama daraja na baadhi ya viongozi au vyama vya siasa kwa ajili
ya manufaa yao, bali amewataka wazitumia fursa na rasilimali zilizopo
kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Dr.
Chimbi ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa
Tanganyika ambayo kimkoa yalifanyika wilayani Bahi katika Kijiji cha
Mkakatika ambako jumla ya vijana hamsini (50) wa Chama cha Ushirika wa
Vijana wa Vyuo Vikuu wa Kilimo na Masoko walikutana kwa lengo la
kusafisha eneo lenye ukubwa wa ekari 50 walilotengewa na Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi kwa ajili ya Kilimo ikiwa ni jitihada za serikali
kuwawezesha vijana kujiajiri.
"Vijana
kwa sasa ni wakati wa ninyi kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko
maslahi yenu binafsi...hivyo kupitia kilimo mtakachoendesha katika eneo
hili, ni matumaini yangu kuwa kwa faida mtakayopata mtakuwa chachu ya
maendeleo na mabadiliko kwa vijana wengine nchini". Alisema Dr. Nchimbi.
Aidha,
Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Dodoma
kuhakikisha kuwa maadhimisho ya sherehe za kitaifa kama hizo kutofanyika
majukwaani kwa viongozi kushuhudia ngoma na burudani nyingine wakati ni
muda wa kutekeleza MATOKEO MAKUBWA SASA, badala yake wawaongoze vijana
katika fursa na rasilimali zilizopo na namna zitakavyowakwamua kiuchumi.
Ambapo kwa kufanya hivyo, vijana wataendelea kuuenzi uhuru huo kwa
vitendo.
Pamoja
na hayo, Dr. Chimbi aliendesha harambee kwa viongozi mbalimbali
waliofika katika maadhimisho hayo kwa ajili ya kuchangia fedha za
kuwasaidia vijana hao kusafishia shamba hilo, ambapo zilipatikana
shilingi 1,650,000.00.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ilikuwa ni "Vijana ni nguzo ya rasilimali watu, tuwaamini na tuwatumie kwa manufaa ya taifa letu"
No comments:
Post a Comment