DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, August 19, 2014

RC DODOMA DR. REHEMA NCHIMBI AFUNGUA JENGO LA HUDUMA KWA WAGONJWA WA NJE (OPD) WILAYANI MPWAPWA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikata utepe kufungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) kwenye Kituo cha Afya cha Lumuma Mpwapwa mwishoni mwa juma lililopita, kushoto  ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Christopher Kangoye na kulia ni Bw. Anjelo Dauria Mwenyekiti wa Shirika la Marafiki wa Lumuma la Italia waliofadhili Milioni 350  za ujenzi wa jengo hilo. Kituo cha Lumuma Mpwapwa  kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Dodoma kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) kwenye Kituo cha Afya cha Lumuma wilayani Mpwapwa mwishoni mwa juma lililopita. Jengo hilo lina  thamani ya milioni 350,  kituo hicho kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Dodoma kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema, kushoto ni Mkuu wa Shirika hilo Sr. Florencia Mbeyu.


Muonekano wa jengo la OPD kwenye Kituo cha Afya cha Lumuma Mpwapwa lililogharimu milioni 350 kwa ufadhili wa Shirika la Marafikii wa Lumuma la Italia, jengo hilo lina idara zote muhimu zinazohitajika kwa ajili ya wagonjwa wa nje, lilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dr Rehema Nchimbi mwishoni mwa juma lililopita.

Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dr Rehema Nchimbi (kulia ) akiserebuka kwaito kusherehekea na baadhi ya vijana wa Kata ya Lumuma wilayani Mpwapwa waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la OPD kwenye Kituo cha Afya cha Kata hiyo mwishoni mwa juma lililopita.
Makamu wa Askofu Kanisa Katoliki Dodoma, Padri Chesco Msaga (wa pili kulia) akiendesha misa takatifu kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la OPD kwenye Kituo cha Afya cha Lumuma wilayani Mpwapwa kituo ambacho kinamilikiwa na kanisa hilo kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema.

Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la Rehema na mama yake kama ishara ya kumuenzi Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuwa mtoto huyo alizaliwa kwenye Kituo cha Afya Lumuma wilayani Mpwapwa majira ambayo kiongozi huyo alikuwa ndio anawasili kituoni hapo kufungua jengo la OPD lililogharimu kiasi cha milioni 350 mwishoni mwa jjuma lililopita.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi, viongozi wa Kanisa Katoliki na Shirika la Watawa la Mt. Gema Dodoma na marafiki wa Lumuma raia kutoka Italia ambao ndio waliofadhili ujenzi wa jengo la OPD kwenye Kituo cha Afya cha Lumuma wilayani Mpwapwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.

Umati wa wananchi wa Kata ya Lumuma wilayani Mpwapwa na maeneo ya jirani ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la OPD kwenye Kituo cha Afya cha kata hiyo.

No comments:

Post a Comment