Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.
Taasisi
ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali
mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, mkoani Shinyanga
ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban
300.
Misaada
hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali
za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya
kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi
vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo
imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo zimetolewa
na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji ya watu
wenye ualbino kwa njia ya elimu. |
No comments:
Post a Comment