Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa
Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal
Investigation).
Kabla ya
uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia
ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S.
Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais Kikwete pia
amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola kuongoza Idara
ya Intelijensia ya Jinai, kujaza nafasi inayoachwa na Kamishna Msuya.
Kabla ya Uteuzi huu, DCP Mlowola alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Mei, 2015
Imetolewa na;
Premi Kibanga, Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Ikulu – Dar es Salaam. 12 Mei, 2015
|
No comments:
Post a Comment