Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty C. Mkwasa akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake juzi baada ya kumkamata baba aliyemuoza binti wa miaka 13 (Jina limehifadhiwa) kwa mbuzi 11 ambapo baadaye binti huyo aliamua kutoroka kutokana na kushindwa kuhimili ndoa hiyo kwa umri alionao na kusema kuwa kitendo alichofanyiwa ni unyanyasaji mkubwa wa kijinsia. Binti huyo kwa takriban mwezi mmoja sasa anaishi na Mkuu huyo wa wilaya nyumbani kwake kwa matarajio ya kumsomesha huku baba yake Ndahani Mtemi anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani hapo ili sheria ichukue mkondo wake. |
No comments:
Post a Comment