Chama cha wafanyakazi wa hifadhi, mahoteli, majumbani, huduma za jamii
na ushauri (CHODAWU) kimeiomba serikali ya Tanzania kuridhia mkataba wa
wafanyakazi wa majumbani wa kazi zenye staha namba 189 uliopitishwa
kimataifa na shirika la kazi Duniani ILO mwaka 2011 ili uanze kutumika
katika sheria zetu za nchi.
Mkataba huo wenye mapendekezo 201 umelenga zaidi kuhakikisha wafanyakazi wa majumbni wanapata haki zao za msingi katika sehemu za kazi na mazingira mazuri ya kazi wanazofanya hii ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vyama vya wafanyakazi, kupata mishahara iliyoidhinishwa kisheria, kupata mikataba ya ajira, kupata likizo za mwaka, uzazi na ugonjwa halikadhalika kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii.
Hayo yalisemwa leo hii na katibu wa CHODAWU Mkoa wa Dodoma Bi. Atupakisye Mtafya alipokuwa akitoa taarifa ya CHODAWU wakati wa mkutano wa kuzindua kampeni ya kitaifa kwa njia ya vyombo vya habari juu ya kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbani uliofanyika mjini Dodoma leo hii.
Akizungumzia kampeni hiyo inayofanywa kwa njia ya vyombo vya habari Bi. Atupakisye amesema kuwa lengo la kampeni ni kuipa jamii uelewa juu ya mkataba namba 189 wa kazi zenye staha kwa wafanyakazi majumbani, sheria za kazi na kusisitiza mazingira bora ya kazi. Amewataja wafanyakazi wa majumbani kama kundi kubwa ambapo kwa takwimu za ILO mwaka 2008 idadi ya wafanyakazi za majumbani ilikuwa milioni 5.2 na kusisitiza kuwa wanastahili haki kama wafanyakazi wengine.
Bi Atupakisye alibainisha kuwa wafanyakazi wa majumbani wanamchango mkubwa katika familia na uchumi wa nchi kwa kazi wanazofanya majumbani na pia kwa kuwapa fursa wafanyakazi wengine kufanya kazi za uzalishaji katika sekta rasmi na zisizo rasmi kwa ufanisi. Aliongeza kuwataka waajiri wazingatie viwango vya ajira vilivyoainishwa katika sheria ya ajira na mahusiano kazini pamoja na sheria ya taasisi za kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakati akizindua rasmi kampeni hiyo ya kuhamasisha kwa tumia vyombo vya habari aliwataka CHODAWU kuwa na mkakati wa kuanza na waajiri kwa kuwahamasisha watambue na kutekeleza haki za wafanyakazi majumbani kwani endapo wao hawatahamasika basi manyanyaso na uvunjifu wa haki ya wafanyakazi majumbani yataendelea kuwepo hata kama serikali itaridhia mkataba huo namba 189.
Dr. Nchimbi pia amewataka CHODAWU ktk kampeni yao ya kutaka serikali iridhie mkataba namba 189,wajaribu kuangalia na kutofautisha historia, mazingira,mikao ya kisera, ameelezea mkao wa mahoteli ni wa kiuchumi wakati wafanyakzi majumbani ni wakujikimu zaidi. Vilevile alisisitia tofauti za kutoa huduma muhimu kwa wafanyakazi ziangaliwe kwa kutoa mfano kuwa ni vigumu utoaji wa huduma kwa wafanyakazi ufanane kati ya familia ya watu kama walimu wa shule za msingi na mameneja au wakuu wa taasisi na mashirika/makampuni kwa kuwa hata vipato vyao havifanani.
Dr. Nchimbi mbali na kutambuaa umuhimu wa wafanyakazi wa majumbani kwa kazi zao wanazofanya majumbani pia ameonesha kutambua umuhimu mkubwa wa sekta ya ajira majumbani n kusema kuwa sekta ya ajira rasmi haina fursa nyingi kama sekta zisizo rasmi. Vilevile aliwaasa waajiri hususani wakinamama wenye tabia za kujisahau majumbani kuwaachia majukumu yote wafanyakazi wao nyumbani kuwa tabia hio imechangia kuvurug a familia zao kwani kumeibuka tatizo la waume zao kuanzisha mahusino ya kimapenzi/kiunyumba na wasaidizi majumbani.
Kwa upande wake mwakilishi wa ILO ambao ndio wafadhili wa kampeni ya kuhamasisha kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa majumbaniaba kupitia vyombo vya habari Bi. Kokushubila Kabanza alijulisha kuwa wafanyakazi wa majumbani wamesahaulika sana na sheria zake za kazi hazitekelezwi hivyo kuitaka serikali nayo kuungana na nchi nyingine wanachama kuridhia mkataba namba 189 na kusema kuwa mpaka sas ni mataifa 10 tu wanachama ndio wameridhia Afrika Kusini na Moroko zikiwemo kw a upande w a Nchi za kiafrika na kuongeza kasi ya nchi wanachama kuridhia bado ni ndogo sana.

No comments:
Post a Comment