.........................................................................................................................................
Mkuu wa
mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amelitaka shirika la posta Mkoa wa Dodoma
kuhakikisha wananchi wa kawaida wanafikiwa na huduma mpya ya posta ya haraka ya
kukusanya na kusambaza nyaraka, vipeto na vifurushi mjini Dodoma inayofahamika
kama City Urgent Mail-pCUM ili jamii kuanzia ngazi ya mwananchi wa kawaida
ifaidike na huduma hiyo.
Dr Nchimbi aliyasema hayo mapema jana kwenye viwanja vya ofisi za posta mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya posta duniani yaliyokwenda sambamba na uzinduzi wa huduma hiyo mpya ya posta. Dr. Nchimbi alilitaka shirika la posta kutowatazama
Dr Nchimbi aliyasema hayo mapema jana kwenye viwanja vya ofisi za posta mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya posta duniani yaliyokwenda sambamba na uzinduzi wa huduma hiyo mpya ya posta. Dr. Nchimbi alilitaka shirika la posta kutowatazama
makampuni makubwa pekee ya kibiashara,taasisi za
serikali,mashirika na wafanyabiashara wakubwa bali wahakikishe huduma hiyo
inawafikia hadi wananchi wa kawaida kwani huduma hiyo ina umuhimu wa kipekee
kwa makundi hayo yote.
Aliongeza kuwa wakati umefika wa shirika la posta kuingia mashirikiano na
mashirika/makampuni/taasisi zinazotoa huduma kwa jamii kama mabenki, kampuni za
simu, mamlaka za maji safi na salama na nyinginezo ili kuongeza ufanisi katika
kuwahudumia wananchi. Alisema kuwa kwa kiasi kikubwa huduma hii inarahisisha
utendaji,inaokoa muda na hivyo inaongeza ufanisi na tija katika kutoa huduma
kwa watu.
Dr Nchimbi pia aliwasisitiza wananchi w mkoa wa Dodoma wajasiriamali,taasisi
mbalimbali za serikali na zisizo za serikali kuichangamkia huduma hiyo kwani ni
ya gharama nafuu,inaokoa muda na kuleta ufanisi na iko wazi kwa mtu wa aina
yoyote na shughuli za aina yoyote ya halali. Katika hatua nyingine aliwaagiza
mamlaka ya mawasiliano TCRA Mkoa wa Dodoma, kwa kushirikiana na Ofisi ya
Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Dodoma na Mamlaka ya ustawishaji makao
makuu chini ya uongozi wa ofisi ya mkuu wa wilaya Dodoma Mjini kuona namna ya
kukamilisha anuani za mitaa na namba za majengo ili huduma hiyo mpya ya posta
iweze kufanyika kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake meneja wa posta mkoa wa Dodoma Bi. Margreth Mlyomi aliuambia
umma wa wananchi na wadau wa posta mkoa wa Dodoma kuwa posta imekuwa na uzoefu
wa kuendesha shughuli zake kwa usiri mkubwa wa nyaraka na mizigo mbalimbali n a
hivyo huduma hii mpya ya pCUM itazingatia sana usiri na ufanisi hususani wa
muda na hivyo wadau waichangamkie.
Nae meneja wa huduma ya barua za haraka-EMS kutoka posta makao makuu Ndg. John
Tinga alibainisha kuwa huduma hiyo ya pCUM imeanza hapa nchini tangu
mwaka 2004 na hadi sasa inapatikana kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo
Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Zanzibar na sasa imepiga hodi Mkoa wa Dodoma na
kuongeza kuwa maeneo yote ilipotangulia huduma hiyo imeonekana kuleta ufanisi
mkubwa.
No comments:
Post a Comment