MAMLAKA
YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI DODOMA
TAARIFA
KUTOKA DUWASA
Mamlaka ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma imekuwa ikiathirika katika uzalishaji na
usambazaji majisafi kwa wateja wake kutokana na makatizo ya umeme wa TANESCO ya
mara kwa mara jambo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu kwa wateja kwa
kukosa huduma muhimu ya maji.
Kwa takwimu, katika
kipindi cha mwezi Oktoba 2008 hadi mwezi Oktoba 2013 DUWASA haikuzalisha,
kusukuma na kusambaza majisafi kwa wateja wake kwa jumla ya saa 1,548 kutokana na Makatizo ya umeme wa TANESCO kwenye visima
na mitambo ya kuzalisha na kusukumia majisafi ambao ulikatika kwa jumla ya saa
1,548. Makatizo hayo ya umeme kuanzia mwezi Oktoba 2008 hadi Oktoba 2013
yamesababisha DUWASA kutozalisha majisafi kiasi cha mita za ujazo 2,012,400
sawa na lita 2,012,400,000 (lita bilioni mbili kumi na mbili milioni na mia nne
elfu).
Maeneo
mengi ya mji yamekuwa yakiathirika na upatikanaji wa majisafi kufuatia makatizo
hayo ya umeme.
Eng.
Peter A. Mokiwa
MKURUGENZI MTENDAJI
DUWASA
No comments:
Post a Comment