DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, October 23, 2013

RC DODOMA AWAONGOZA MAMIA YA WAPIGANAJI WA JWTZ KANDA YA DODOMA KUUAGA MWILI WA HAYATI MEJA ANTHONY IGOBEKO


Baadhi ya wapiganaji wa Jeshi la Wananchi JWTZ Kanda ya Dodoma  walijitokeza kuuaga Mwili wa Marehemu Meja Igobeko.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa hayati Meja Anthony Igobeko aliyefariki Oktoba 18  baada ya kuugua kiharusi. Ibada ya  kuuaga mwili wa marehemu ilifanyika juzi kwenye kambi ya  jeshi Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma  na baadae mwili ulipelekwa Dar es salaam kwa maziko.

Mkuu wa Jeshi kanda ya Dodoma Brigadia Masumbuko Mdeme akitoa salamu za mwisho kwa Mwili wa hayati Meja Anthony Igobeko aliyefariki Oktoba 18 baada ya kupata kiharusi. Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilifanyika juzi kwenye kambi ya jeshi Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na baadae mwili ulipelekwa Dar es sallaam kwa maziko.

Baadhi ya Ndugu  wa karibu wa Hayati Meja Anthony Igobeko waliohudhuria Ibada ya kumuaga iliyofa nyika jana kwenye Kambi ya Jeshi ya Ihumwa iliyopo nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

Mwili wa marehemu Meja Anthony Igobeko ukiwa umebebwa kwenda kupakiwa kwenye gari tayari kuusafirisha kwenda Dar es salaam kwa maziko, kushoto ni  Mkuu wa Jeshi kanda ya Dodoma Brigadia Masumbuko Mdeme na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi wakishuhudia.

Buriani Meja Anthony Igobeko, Jeshi na Nchi yetu itakukumbuka kwa utumishi wako wa muda mrefu na uliotukuka.


.........................................................................................
 
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki aliwaongoza mamia ya maafisa ngazi za juu,chini na wapiganaji waJeshi la Wananchi JWTZ kuuaga mwili wa aliyekuwa mmoja kati ya wakuu wa vikosi vya Jeshi Mkoani Dodoma hayati Meja Anthony Igobeko aliyefariki Oktoba 18 kufuatia kuugua kiharusi.

Ibada ya kuuaga Mwili wa Hayati Meja Igobeko tayari kwa kuusafirisha kuelekea Dar es salaam  ilifanyika jana kwenye kambi ya Jeshi Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma. Kwa upande wake Kapteni Manyiga wakati akitoa taarifa kwa umma uliokusanyika kumuaga hayati Meja Igobeko, alisema kuwa Meja Igobeko hakuwa katika hali ya kuugua wala kusumbuliwa kiafya isipokuwa Oktoba 18 asubuhi alipata kiharusi na kufariki majira ya mchana.

Akimuelezea hayati Meja Igobeko , Mkuu wa Jeshi kanda ya Dooma Brigadia Masumbuko Mdeme alisema kuwa Meja Igobeko alikuwa Mpiganaji Mahiri, Afisa Mkuu Mwadilifu, mtiifu na hodari,alikuwa mwepesi kutekeleza amri; kwa ujumla alikuwa na sifa za kiongozi na kuwa Jeshi limepata limepata pigo.

Akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa Mkoa wa DodomaDr. Rehema Nchimbi alisema kuwa majonzi hayaendi kwa wanandugu pekee bali  ni kwa mkao mzima wa Jeshi. Amelitaka jeshi kuikabili hali hiyo akionesha imani kubwa aliyonayo kwa jeshi-JWTZ, aidha amelitaka  Jeshi kuendelea kujipanga na kuongeza ufanisi.

Akiwaasa mamia yawapiganaji waliokusanyika Kambini hapo kuuaga mwili wa mpiganaji mwenzao, amewataka wote kumuenzi Hayati Meja Igobeko kwa kuishi na kufanya yale mazuri ya mfano aliyoyafanya Meja Igobeko enzi za Uhai wake.

Akitoa salamu za familia, mwakilishi wa familia ya marehemu Igobeko Ndg. Emmanuel Masaga alilishukuru Jeshi kwa kumlea ndugu yao na kumuhangaikia sana wakati alipopata kiharusi na kusema kuwa hiyo inaonesha kuna ushirikiano mkubwa na upendo katika jeshi la wananchi wa TAnzania.

Akitoa wasifu wa Marehemu Meja Igobeko, Kapteni Manyiga alisema kuwa marehamu alizaliwa mwaka 1959 mkoani Mwanza, alijiunga na jeshi  mwaka 1980 na alikuwa wa mfano Jeshini, alikuwa na ustawi mzuri hadi kufikia ngazi ya Meja mwaka 1995. Vilevile alishatunukiwa nishani mbalimbali zikiwemo miaka 40 ya Jeshi la Wananchi JWTZ, utumishi wa muda mrefu na utumishi uliotukuka. Aliongeza kuwa marehemu ameacha mke na watoto 4.

No comments:

Post a Comment