Serikali ya Ujerumani imesema mfumo wa mawasiliano wa Kansela
Angela Merkel uko salama licha ya madai kuwa mashirika ya kijasusi
ya Marekani yalidukua mawasilano yake ya simu yake ya
mkononi.
Ufichuzi wa kuwa Shirika la Usalama la Taifa la Marekani
(NSA) limekuwa likidukua mawasiliano ya raia wa bara la Ulaya na
viongozi wake, limezorotesha uhusiano kati ya Marekani na
washirika wake wa Ulaya.
Ujerumani na Brazil zinatarajiwa
kuwasilisha azimio katika Umoja wa Mataifa pengine hata wiki ijayo
la kutaka kupanuliwa kwa haki za kuwa na faragha katika
mawasiliano ya mitandaoni na kumtaka Kamishna wa Kaki za Binadaamu wa umoja huo kulizingatia suala hilo.
Hapo jana gazeti
moja la Uingereza liliripoti kuwa NSA ilidukua mawasiliano ya simu ya
viongozi 35 kote duniani kundi la viongozi linalomjumuisha
Merkel.Ujerumani itawatuma maafisa wake wakuu wa kijasusi
kwenda katika Ikulu ya Marekani ya White House wiki ijayo, kutafuta
majibu juu ya madai kwamba Marekani ilinasa mawasiliano ya simu
ya mkononi ya Kansela Merkel. (Habari hii kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani)
No comments:
Post a Comment