DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, August 31, 2015

LOWASSA ATIKISA IRINGA!

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa  wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Mkoani Iringa jana Agosti 30, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, William Joseph Mungai, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa jana Agosti 30, 2015.
Waziri wa zamani wa Elimu, Mh. Joseph Mungai akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa jana Agosti 30, 2015.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa jana Agosti 30, 2015.
 Mkazi wa Iringa mjini ambaye anahitaji mabadiliko.

 Umati wa Wakazi wa Mji wa Iringa Mjini ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Sabasaba, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, jana Agosti 30, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsalimia kijana mwenye ulemavu (jina lake hakupatikana kwa haraka) aliyehudhulia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea huyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Iringa Mjini, leo Agosti 30, 2015

IS WALIPUA MADHABAHU SYRIA

Madhabahu yakilipuliwa
Shirika hilo limesema kuwa uharibifu mkubwa umetokea baadha ya shambulio hilo.
Wiki iliyopita wanamgambo hao wameoneshwa aktika video wakilipua hekalu nyingine ya kale ya Baalshamin. Islamic State waliuteka mji wa Palmyra mwezi Mei na kuzua hofu ya kushambuliwa madhabahu hayo.
Madhabahu ya Palmyra
Wapiganaji wa dola ya kiislamu IS, wanadaiwa kulipua sehemu ya madhabahu ya kidini katika mji wa Syria wa Palmyra.
Kundi la kutetea haki za binadamu nchini Syria limesema kuwa wanamgambo hao wametumia mabomu kulipua hekalu ya kiroma ya Bel.

MAGUFULI AUNGURUMA LUDEWA, ASEMA FILIKUNJOMBE NI MAGUFULI AJAYE

Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM John Pombe Magufuli akimsikiliza Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa aliyepita bila kupingwa kueleza matatizo yanalolikabili jimbo hilo.
Katikati ni John Pombe Magufuli mgombea Urais CCM, Kushoto ni Deo Filikunjombe aliyepita bila kupingwa Jimbo la Ludewa, na kulia ni Khamis Kayombo mgombea udiwani CCM Kata ya Mlangali.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe aliyepita bila kupingwa akizungumzia jimboni humo akisisitiza jambo.
Waziri wa nyumba, ardhi na makazi, Willium Lukuvi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Filikunjombe akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mlangali. Picha kwa hisani ya MjengwaBlog

KAULI ZA MOURIHNO BAADA YA KUPOKEA KICHAPO KUTOKA KWA CRYSTAL PALACE

Sherehe za kutimiza michezo 100 kwa Jose Mourinho katika dimba la Stamford bridge ziliharibiwa na kichapo kutoka kwa Crystal Palace. Kilikua kichapo cha kwanza kwa Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani wa Stamford bridge tangu April 2014  na kichapo cha pili  kwa Mourinho katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge katika michezo 100 aliyoitimiza jana.
Katika mkutano na waandishi wa habari Mourinho alisema “Walikuja na kila kitu walichokua nacho, timu yao ilikua imejianda, wachezaji wao walikua wamejiandaa, walikuja na morali ya ajabu. Walikua na bahati lakini walistahili hiyo bahati na waliipigania”
“Nahisi tulistahili zaidi. Sisemi kwamba tulistahili kushinda sababu sio kweli, ila tulistahili”
Mourinho alilaumu baadhi ya wachezaji wake kwa kuonesha kiwango cha chini katika mechi hiyo ili kuweza kutetea ubingwa wao.
“Golikipa na mabeki wangu wawili wa kati walikua katika kiwango kizuri sana, tulitengeneza nafasi nyingi ila kuna baadhi ya wachezaji hawakua kwenye mchezo. Katika hatua hii unavyokua na mpinzani mzuri aliyejipanga na ana morali ya hali ya juu, hana cha kupoteza unahitaji watu wafanye kazi. Siwezi sema nilikua na wachezaji 11 waliokua wanacheza kwa wakati mmoja” Mourinho alisema.
“Wachezaji wawili au watatu walicheza chini ya kiwango na nina jilaumu kwa kumuacha mmoja wao acheze kwa dakika 90. ”
Ushindi wa Manchester City yenye point 12 unafanya kue na tofauti ya point 8 kati yao na Chelsea yenye point 4. Lakini Mourinho amesema hilo haliwatoi katika mbio za ubingwa.
“Tunatofauti ya point 8 na anaeongoza ligi na ingekua kwenye ligi nyingine ningesema tushapoteza ubingwa sababu katika hizo ligi inakua ni vigumu  kwa timu za juu kupoteza point nyingi hivyo. Ila katika ligi ya uingereza  sisemi kama ligi imeisha. ”
“Ukweli ni kwamba tumeanza ligi vibaya, point nne katika michezo minne ni mwanzo mbaya sana”. Picha na Habari kwa hisani ya ShaffihDauda.co.tz

UKAWA WAZINDUA RASMI KAMPENI JANGWANI!


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015. 



 Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, Agosti 29, 2015.
Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, Agosti 29, 2015.

Friday, August 28, 2015

DKT. MAGUFULI ANADI SERA TUNDUMA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana, kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyia Oktoba 25  mwaka huu.
Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza  kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mkoani Mbeya.
Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni.

BAWACHA: ITAHAMASISHA WANAWAKE NCHINI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU, 2015

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya uzinduzi wa kongamano la kuunganisha wanawake ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu Octoba 25. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega na Makamu Mwenyekiti, Hawa Mwaifunga.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa kampeni ya wanawake kupitia kongamano litakalofanyika leo katika ukumbi wa Millenium Tower. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Bavicha, Grace Tendega. 
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama juu ya uzinduzi wa kongamano la kuunganisha wanawake ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu Octoba 25. 
Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega akifafanua jambo.
Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee.

Tuesday, August 25, 2015

ARSENAL YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI, YATOA SARE TASA NA LIVERPOOL EPL

Augosti 24 klabu ya Arsenal ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Liverpool katika mechi ya Ligi Kuu Uingereza mechi iliyochezwa katika uwanja wa Emirates wenye  uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 60,000. Mechi hiyo ambayo ilikuwa na mvuto wa aina yake kwa mashabiki wa Ligi Kuu Uingereza. Mashabiki walikuwa na kiu ya kukosa mechi za Ligi Kuu kwa muda ila kwa bahati mbaya mechi hiyo ya Arsenal dhidi ya Liverpool imemalizika kwa sare ya kutofunga goli (0-0).





Picha zote kwa hisani ya millardayo.com

PEDRO AAGA RASMI FC BARCELONA

Winga mshambuliaji mpya aliyejiunga na Klabu ya Chelsea 'The Blues' siku chache zilizopita akitokea katika Klabu ya FC Barcelona ya Hispania Pedro Rodriguez, August 23 alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu yake mpya ya Chelsea na kufanikiwa kufunga goli. Ndani ya saa 24 toka Pedro afunge goli amerudi katika klabu yake ya zamani ya FC Barcelona kuaga rasmi wachezaji wenzake wa zamani, Pedro alipewa muda wa kwenda kuaga katika klabu ambayo ameitumikia kwa takribani miaka 10.

Pedro akiwa katika chumba cha kukutana na vyombo vya habari ambako kulikuwa na wachezaji zaidi ya 20 wakimuaga akiwemo MessiNeymar na Gerard Pique. Siku kadhaa zimepita toka Pedro Rodriguez ajiunga na klabu ya Chelsea akitokea klabu ya FC Barcelona ya Hispania kwa dau la pound milioni 21.4. Hivyo, alirudi Hispania kuaga wachezaji wenzake ambao wengine ameishi nao katika kipindi cha zaidi ya miaka 6.

RONALDO ATISHA!

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid yaHispania Cristiano Ronaldo amefanikiwa kununua jumba la kifahari lililopo katika mji waNew York Marekani kwa dola za kimareka milioni 18 ambazo ni zaidi ya bilioni 30 za Kitanzania. Inaripotiwa kuwa wazo la Ronaldo kununua nyumba hiyo alilipata kutoka katika novel ya’50 Shades of Grey’ hata hivyo ununuaji wa nyumba hiyo kwa Ronaldo unaongeza uvumi kuwa huenda ana mapngo wa kwenda kucheza katika Ligi Kuu Marekani kabla hajastaafu soka.








Chumba cha kulala
Ukiwa juu muonekano wa maeneo jirani.
Picha zote ni kwa hisani ya millardayo.com