DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, August 25, 2015

LOWASSA AZUNGUKA DAR KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam jana, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mhe. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar. 
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akiwa katikati ya umati wa watu wakati alipotembelea eneo la Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam jana.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam, mapema jana asubuhi. 
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anaeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA), Mhe. Edward Lowassa akilipa nauli ya daladala alilopanda Kituo cha Gongolamboto mwisho kuelekea Chanika, jijini Dar es Salaam jana alipokuwa kwenye  ziara ya kujionea hali halisi ya shida ya usafiri wa umma (daladala) jijini humo.
Mhe. Lowassa akishuka kwenye daladala.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliokuwa kituoni hapo kusubiria usafiri.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa akizungumza na Vijana wanaojihusisha na shughuli mbali mbali katika kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoa ya Lindi na Mtwara, kilichopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala.


Wakazi wa mji wa Mbagala wakiushangilia msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakati walipotembelea Kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es salaam, wakati walipotembelea kituo hicho jana. Picha zote na Othman Michuzi.

No comments:

Post a Comment