DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, August 25, 2015

PEDRO AAGA RASMI FC BARCELONA

Winga mshambuliaji mpya aliyejiunga na Klabu ya Chelsea 'The Blues' siku chache zilizopita akitokea katika Klabu ya FC Barcelona ya Hispania Pedro Rodriguez, August 23 alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu yake mpya ya Chelsea na kufanikiwa kufunga goli. Ndani ya saa 24 toka Pedro afunge goli amerudi katika klabu yake ya zamani ya FC Barcelona kuaga rasmi wachezaji wenzake wa zamani, Pedro alipewa muda wa kwenda kuaga katika klabu ambayo ameitumikia kwa takribani miaka 10.

Pedro akiwa katika chumba cha kukutana na vyombo vya habari ambako kulikuwa na wachezaji zaidi ya 20 wakimuaga akiwemo MessiNeymar na Gerard Pique. Siku kadhaa zimepita toka Pedro Rodriguez ajiunga na klabu ya Chelsea akitokea klabu ya FC Barcelona ya Hispania kwa dau la pound milioni 21.4. Hivyo, alirudi Hispania kuaga wachezaji wenzake ambao wengine ameishi nao katika kipindi cha zaidi ya miaka 6.

No comments:

Post a Comment