DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, August 25, 2015

DKT. MAGUFULI ARINDIMA MKOANI KATAVI: HAPA KAZI TU!


Mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akimwaga sera katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi jana ikiwa ni siku ya pili ya kampeni zake alizozindua viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam juzi. 
Dkt. Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  kabla ya kupanda jukwaani kuhutubia mjini Mpanda jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia kabla ya kumtambulisha Mgombea urais wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Mishimo, Mpanda mkoani Katavi jana.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimtambulisha Dkt. Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya  Katumba, wilayani Nsimbo.
Dkt. Magufuli akijinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Azimio  mjini Mpanda jana.
Ni furaha iliyoje kwa wananchi wakati Dk. Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Mpanda jana.
Sehemu ya umati wa wananchi  wakimsikiliza Dk John Magufuli katika Kata ya Mishimo.

No comments:

Post a Comment