Wapiganaji wa Islamic State
***
Mtaalamu wa masuala
ya silaha za kemikali katika wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq
amekamatwa na vikosi maalum vya Marekani na sasa anahojiwa.
Mtu
huyo alikuwa mtaalamu wa masuala ya silaha za kibaiolojia wa aliyekuwa
rais wa Iraq Sadam Hussein ,aliyepinduliwa na uvamizi wa Marekani nchini
Iraq mwaka 2003, duru za Iraq na zile za Marekani zimeambia vyombo vya
habari vya Marekani.
Akijulikana kama Sleiman Daoud Al_fari,aliripotiwa kukamatwa mwezi uliopita.
Hatahivyo, msemaji
wake amesema kuwa vikosi maalum vya Marekani vimeanza oparesheni zake
nchini Iraq, ikiwa ni mwanzo wa vita vikali dhidi ya Islamic State.
Mtu
huyo amewaambia wanaomuhoji vile kundi la Islamic State lilivyotumia
gesi ya sumu katika makombora yake, duru za Marekani zimeliambia gazeti la
"The New York Times". CHANZO: bbcswahili.com |