Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta nchini kuanzia leo Machi 2, 2016.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana
mchana, Mkurugenzi Mkuu wa (EWURA), Felix Ngamlagosi alisema bei
ya Petroli imeshuka sh. 31 kwa lita sawa na asilimia 1.70, Dizeli sh.
114
kwa lita sawa na asilimia 7.10 na mafuta ya taa kwa sh. 234 kwa lita sawa na asilimia 13.75 ikilinganishwa na mwezi uliopita.
Alisema
hapa nchini kwa sasa Petroli itauzwa Sh.1,811, Dizeli sh. 1,486 na
mafuta ya taa sh. 1,465. Alisema kupungua kwa bei hizo kwa soko
la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko
la dunia.
Hata
hivyo alisema hakutakuwa na mabadiliko yeyote ya bei ya petroli na
dizeli kwa mkoa wa Tanga kwa mwezi huu na kwamba hiyo imetokana na
kutopokea mafuta mapya kupitia Bandari ya mkoa huo katika kipindi
cha Februari mwaka huu.
“Mamlaka
inapenda kuujulisha umma kuwa bei hizi kikomo za mafuta kwa eneo husika
zinapatikana vilevile kupitia upigaji wa simu ya mkononi kwa mitandao
yote kwenda namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.
Aliongeza
kuwa kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za
mafuta zitaendelea kupangwa na soko hivyo Ewura itaendelea kutoa taarifa
za bei kikomi lengo likiwa ni kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki
kuhusu manunuzi ya bidhaa hiyo.
Aidha
amevitaka vituo vyote vya mafuta nchini na kuchapisha bei za bidhaa za
mafuta katika mabango yanayonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta,
punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo
husika.
Alisema
wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo
vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni
kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa
wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.
Alibainisha
kuwa wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya
malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta kwa lita na
kwamba stakabadhi ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa
mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya
juu kuliko bei kikomo, au yenye kiwango cha ubora kisichofaa. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
|
Wednesday, March 02, 2016
EWURA YATANGAZA RASMI KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment