Mamia ya watu walimiminika kushuhudia jua likinaswa na mwezi.
***
Hoteli zilizopo katika maeneo mazuri ya kushuhudiwa
jua likinaswa zilijaa miezi kadhaa iliopita na katika baadhi ya maeneo
ilibidi maafisa watafute nafasi za ziada kwa watalii waliokuwa kwenye
maboti.
Katika kisiwa cha Belitung mamia ya wageni na watalii wa
nchni walikusanyika katika fukwe za bahari kabla ya alfajiri. Wakati jua
lilipoanza kunaswa na mwezi walishangilia na baadaye kunyamaza kimya
kwa mshangao.
Wengi wamelielezea tukio hilo kama 'tukio la
miujiza'. Kwa wengi Indonesia, tukio hilo linashirikishwa sana na dini
na watu huomba, sherehe za kitamaduni na ngoma zimeandaliwa katika
sehemu kubwa la eneo hilo.
Wanasayansi pia wamkuwepo hususan
katika eneo la Maba katika visiwa vya Maluku ambako tukio hilo
limeshuhudiwa kwa dakika tatu, ambao ni muda mrefu kuwahi kushuhudiwa
jua likinaswa na mwezi. CHANZO: BBCSWAHILI.COM |
No comments:
Post a Comment