Ligi ya
Mabingwa barani Ulaya, iliyochezwa usiku wa Machi 09, 2016 kwenye viwanja
viwili tofauti, ikiwemo uwanja wa Stamford Bridge uliyopo jijini
London na Petrovsky uliopo nchini Urusi.
Jiji la
London, wenyeji Chelsea wamelazimika kuchezea
kichapo cha pili mfululizo toka kwa PSG kutoka jijini Paris nchini
Ufaransa kwa kufungwa bao 2-1, ambapo ushindi huo ni kama ule walioupata
timu hiyo ya PSG katika mchezo wao wa awali na kwa maana hiyo, PSG
wameweza kujipatia pointi 6 muhimu na magoli 4, huku Chelsea wao
wakiambulia mabao yao 2.
Kwa hatua
hiyo, PSG anaingia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo mikubwa
kabisa barani Ulaya. PSG ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yoyote ili
kuweza kusonga mbele au sare, hivyo kwa ushindi huo imefuzu hatua ya
robo fainali.
Mchezo mwingine umechezwa nchini Urusi , wenyeji Zenit wameweza kulala kwa bao 2-1 dhidi ya Benfica ya nchini Ureno.
Katika
mchezo wa awali Benfica walikuwa nyumbani na walifanikiwa kushinda bao
1-0, kwa hatua hiyo Benfica wamefanikiwa kuingia hatua ya robo ya
michuano hiyo kwa jumla ya poiti 6 huku ikijipatia mabao 3, dhidi ya
moja la wapinzani wao hao. |
No comments:
Post a Comment