DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, March 10, 2016

MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA SHINYANGA

Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma unaojulikana kwa jina la Public Sector Systems Strenghening (PS3) unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla.
Mkutano wa uzinduzi huo utakaofanyika kwa siku mbili Machi 09,2016 hadi Machi 10,2016 umehudhuriwa na Kiongozi wa timu ya mradi,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,wataalam kutoka kutoka ofisi ya Waziri mkuu na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi,mashirika na taasisi za umma na binafsi-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yupo eneo la tukio ametusogezea picha 30 ,Tazama hapa chini

Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ambaye pia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Public Sector Systems Strenghening(PS3) utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano na utafanya kazi na serikali kuu pamoja na halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

Wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini,wa kwanza kushoto ni Vita Kawawa kutoka wilaya ya Kahama, akifuatiwa na Josephine Matiro kutoka wilaya ya Shinyanga na Hawa Ng’umbi kutoka wilaya ya Kishapu.
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua mradi wa PS3 ambapo alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 13 nchini ambayo itanufaika na mradi huo ambapo alidai umeanza kwa wakati muafaka kwani sasa serikali iliyopo madarakani inataka mabadiliko katika kuhakikisha kuwa serikali inahudumia wananchi ipasavyo.
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) akifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Rufunga alisema mradi huo utakuwa na tija kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Post a Comment