Baada ya wawili hawa kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli amesema wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga hadi Uganda kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki, litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000.
Rais Magufuli ameongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa
bomba la mafuta, pia wamezungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za
jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi
kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali. |
No comments:
Post a Comment